Herbalist Mtaturu
Senior Member
- Aug 17, 2023
- 156
- 237
SABABU ZA MWANAUME KUKOSA MBEGU ZA UZAZI
TATIZO la mwanaume kukosa mbegu za uzazi kitaalam huitwa ‘azoospermia’ au ‘medical condition’. Ni tatizo linaloathiri wanaume wa rika tofauti.
Katika hali hii, mwanaume anakuwa hana mbegu hata moja inayoonekana kwenye manii yake. Hali hii inaweza kusababisha ugumba na utasa kwa mwanaume. Katika hali ya ugumba maana yake linaweza kupatiwa ufumbuzi, lakini inapofikia utasa, uwezo wa kuzaa unakuwa haupo kabisa.
Tatizo la mwanaume kukosa mbegu za uzazi ni kubwa na husababisha ndoa kukosa tiba ingawa kwa kiasi kikubwa lawama huelekezwa kwa mwanamke.
Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, tatizo hili huathiri asilimia moja ya mwanaume, yaani kuwa tasa, kukosa kabisa uwezo wa kuzaa na asilimia ishirini husababisha ugumba kwa wanaume ambapo huweza kutibika baada ya uchunguzi wa kina.
Upungufu wa mbegu za kiume kitaalamu huitwa oligospermia. Hili ni neno linalotumika kuelezea hali ambapo idadi ya mbegu za mwanamme ni ndogo, pungufu ya mbegu milioni 15 katika mililita moja.
Kama hakuna mbegu kabisa, hali hiyo huitwa "azoospermia". Unapohitaji kupata mtoto, idadi ya mbegu unayotoa wakati wa tendo la ndoa ni muhimu. Idadi ya kawaida ya mbegu ni kati ya milioni 15 hadi milioni 200 kwa mililita moja.
VIPIMO
Vipimo vya kuchukua wakati wa kufanya semen analysis:
kuchunguzwa uwingi wa mbegu katika ujazo wa mililita moja. Kisha daktari atataka kujua ni mililita ngapi zinatolewa. Kwa mfano, mtu mwenye mbegu milioni 40 katika mililita na anakojoa mililita moja hawezi kuwa mzuri zaidi ya yule mwenye mbegu milioni 18 kwa mililita na kutoa mililita 4 za ujazo anapokojoa.
Kuchunguza ni asilimia ngapi ya mbegu ambazo zina uwezo wa kutembea, sperm motility, ambapo asilimia 50 ya mbegu kuwa na uwezo wa kutembea kuelekea kwenye nyumba ya uzazi ndicho kiwango cha chini kinachotakiwa.
Ukubwa na maumbo ya mbegu ni kigezo kingine kwa mbegu kuwa na uwezo wa kulirutubisha yai. Uchuguzi unafanyika kuona kuwa ni asilimia ngapi ya mbegu zenye ukubwa na maumbo yaliyokamilika "sperm morphology". Mbegu safi inatakiwa kuwa na asilimia angalau 30 ya mbegu zenye ukubwa na maumbo kamilifu.
Kiwango cha pH cha shahawa ni muhimu vile vile na kiwango kizuri ni cha kati ya pH 7.1 na 8.0. Kiwango kidogo cha pH kinamaanisha mbegu ni za utindikali zaidi na kiwango kikubwa maana yake mbegu ni alkaline. Kiwango cha pH kinaweza kuathiri afya ya mbegu zako na jinsi zitakavyosafiri.
Tatizo hili la kukosekana mbegu za uzazi linasababisha mwanaume kushindwa kumpa mimba mwanamke ndani ya mwaka mmoja wa uhusiano:
Aina za Azoospermia
1️⃣PRETESTICULAR AZOOSPERMIA
Hapa mwanaume anakuwa na korodani zote kama kawaida, lakini hatoi mbegu za uzazi, anatoa manii tu. Tatizo kubwa linakuwa kwenye mfumo wa uchochezi ambapo homoni zake za kiume hushindwa kuchochea uzalishaji, homoni ya FSH inakuwa chini, kiasi kwamba inaathiri uzalishaji wa mbegu.
Tatizo hili linaweza kusababishwa na tatizo katika ubongo ‘hypopituitarism’ na ‘hyperprolactinemia’ na hata matumizi ya dawa za homoni za kiume bila uchunguzi wa kidaktari vinaweza kuathiri uchocheaji.
Chanzo kingine ni wale wanaotumia dawa za kutibu saratani ‘chemotherapy’ ambao huathirika na hali hii. Tatizo hili la uzalishaji kutokuwepo kutokana na matatizo ya homoni pia ni kubwa.
2️⃣TESTICULAR AZOOSPERMIA
Hapa korodani zinashindwa kuzalisha mbegu kutokana na kasoro. Aidha, korodani moja imesinyaa au zote mbili zimesinyaa, yaani ni ndogo sana au kubwa sana, zote au mojawapo, yaani ilimradi umbile la korodani zako si la kawaida, wengine hawana kabisa korodani moja au zote mbili hazipo. Hili ni tatizo kubwa la uzazi kwa mwanaume.
Mwanaume mwenye tatizo hili homoni zake za uzazi zinakuwa juu sana tofauti yule wa mwanzo kwa sababu ya kutokuwepo kwa mfumo wa mrejesho wa taarifa katoka katika ubongo ‘lack of feedback’ inhibition on FSH.
Tatizo hili lipo kubwa kwa asilimia 49 hadi 93 kwa wanaume wenye matatizo ya uzazi ambao hawazalishi mbegu, watakuwa na mojawapo ya kasoro hizo tuizozitaja hapo juu.
Tatizo hili la korodani kushindwa kufanya kazi ya kuzalisha mbegu za uzazi huweza kusababisha mbegu zizalishwe kwa kiasi kidogo sana au zisizalishwe kwa kiasi kidogo sana au zisizalishwe kabisa na zikizalishwa zinakuwa hazijakomaa.
Dalili Za Upungufu Wa Mbegu Za Kiume
➡️Kukosa uwezo wa kumpa mimba mke.
➡️Matatizo katika tendo la ndoa: kwa mfano, kukosa hamu ya tendo la ndoa au matatizo ya uume kusimama kwa muda mrefu ili kukamlisha tendo la ndoa.
➡️Maumivu, uvimbe kwenye maeneo ya korodani
➡️Kupungua kwa nywele za usoni au za mwilini au ishara nyingine za dosari za homoni.
➡️Korodani kusinyaa/,kuingia ndani
wa.me/255656303019
Sababu Za Mwanamme Kuwa na Upungufu wa Mbegu
Tendo la kutengeneza mbegu za mwanamme lina vipengele vingi sana na linahitaji afya nzuri ya korodani na tezi za pituitary na hypothalamus: tezi katika ubongo zinazotengeneza homoni na zinazoruhusu utolewaji wa mbegu. Mbegu zilizotengenezwa ndani ya korodani husafirishwa kupitia mirija myororo hadi zitakapochanganywa na shahawa na kutolewa nje kupitia uume. Tatizo lo lote katika mlolongo huu linaweza kuathiri utolewaji wa mbegu bora.
Kunaweza kujitokeza matatizo katika maumbile ya mbegu au utembeaji wa mbegu. Kwa kawaida ni vigumu kulijua tatizo hili la kuwa na upungufu wa mbegu za kiume.
Varicocele. Varicocele ni kuvimba kwa veni zilizomo ndani ya mfuko wa ngozi unaoshikilia korodani. Hii ni moja ya sababu kubwa ya ugumba kwa mwanamme. Varicoceles husababisha mapungufu katika ubora wa mbegu.
Maambukizi. Baadhi ya maambukizi yanaweza kuathiri uzalishaji wa mbegu au afya ya mbegu au kusababisha makovu yatakayozuia mtiririko wa mbegu. Hii ni pamoja na maambukizi kwenye epididymis (epididymitis) au korodani (orchitis) na baadhi ya magonjwa ya kuambukiza kama gonorrhoea au UKIMWI.
Matatizo Katika Umwagaji Mbegu. Mbegu zaweza kuingia kwenye kibofu cha mkojo (retrograde ejaculation) wakati mwanamme anapofika kileleni badala ya kutoka kupitia uume. Baadhi ya sababu zinaweza kulisababisha hili au kushindwa kutoa shahawa, zikiwa ni pamoja na kisukari, kuumia uti wa mgongo, upasuaji wa kibofu cha mkojo, tezi dume au urethra.
Kuna madawa mengine yanayoweza kuleta matatizo ya umwagaji mbegu, kama dawa za blood pressure zinazojulikana kama alpha blockers.
➡️Kingamwili (Antibodies) kushambulia mbegu. Kingamwili (anti-sperm antibodies), seli za mfumo wa kinga za mwili ambazo kwa bahati mbaya hutambua mbegu kama vivamizi katika mwili na hujaribu kuziharibu.
Uvimbe. Kansa na uvimbe wa aina nyingine usio na madhara vinaweza kuuathiri mfumo wa uzazi wa mwanamme moja kwa moja, kupitia tezi zinazotoa homoni zinazohusiana na uzazi, kama tezi ya pituitary. Upasuaji, mionzi au tiba ya chemotherapy zinazotolewa kutibu uvimbe vinaweza kuathiri uwezo wa mwanamme wa kuzalisha.
Korodani ambazo hazijashuka. Wakati kiumbe akiwa anakua tumboni korodani moja au zote zinaweza kushindwa kuteremka hadi kwenye mfuko wa pumbu kutoka tumboni. Watu wenye hali hii wanakuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kuwa wagumba.
Hormone imbalances. Tezi ya pituitary, hypothalamus na korodani huzalisha homoni muhimu katika utengenezaji wa mbegu mwilini. Mabadiliko katika homoni hizi, na mabadiliko katika mifumo ya tezi za thyroid na adrenal, huathiri uzalishaji wa mbegu.
Matatizo katika mirija ya kusafirisha mbegu. Mirija ya aina nyingi inahusika katika usafirishaji wa mbegu. Mirija hii inaweza kuziba kwa sababu nyingi, ikiwa ni pamoja na kuumia kwa bahati mbaya katika upasuaji, maambukizi au kuota kwa vitu kama cystic fibrosis.
Kuziba kunaweza kutokea kwenye hatua yo yote, ikiwa ni pamoja na ndani ya korodani, kwenye mirija inayotoka kwenye korodani, ndani ya epididymis, ndani ya vas diferens, au ndani ya urethra.
Dosari za chromosome. Dosari za kiurithi kama Klinefelter’s syndrome, ambapo mwanamme anazaliwa akiwa na chromosomes mbili za X na moja ya Y badala ya moja ya X na moja ya Y: zinasababisha ukuaji wa viungo vya uzazi vya kiume usio wa kawaida. Matatizo mengine ya kiurithi yanayohusiana na ugumba ni cystic fibrosis, Kallmann’s syndrome na Kartagener’s syndrome.
Celiac disease. Tatizo katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula linalosababishwa na usikivu wa mwili kwa gluten, ugonjwa uitwao celiac disease unaweza ukasababisha ugumba kwa mwanamme. Ugumba unaweza kuondoka baada ya kula chakula kisicho na gluten.
Baadhi Ya Tiba. Tiba ya Testosterone replacement therapy, matumizi ya dawa za kansa (chemotherapy), baadhi ya dawa za fungus na antibiotics, baadhi ya tiba za vidonda vya tumbo, vinaweza kuathiri utengenezaji wa mbegu na kusababisha ugumba.
Kemikali za viwandani. Kuwa karibu kwa muda mrefu na benzene, toluene, xylene, herbicides, pesticides, organic solvents, rangi na madini ya lead kunaweza kuchangia matatizo ya kuwa mbegu chache.
Metali nzito. Kuwa karibu na lead na madini mengine mazito kunaweza kusababisha ugumba.
Mionzi au X-rays. Kuwa karibu na mionzi kunaweza kupunguza uzalishaji wa mbegu. Inaweza kuchukua muda mrefu kabla uzalishaji haujarudi na kuwa sawa. Mionzi mikali inaweza kusababisha upungufu wa mbegu wa milele
Joto kali kwenye korodani. Joto kali linaharibu uzalishaji wa mbegu na ubora wake. Kuoga maji ya moto, mathalani, kunaweza kupunguza uzalishaji kwa muda fulani. Kukaa kitako kwa muda mrefu, kuvaa nguo za kubana, kufanya kazi kwenye laptop au kompyuta kwa muda mrefu vinaweza kuongeza joto kwenye korodani ma kupunguza uzalishaji wa mbegu.
Matumizi ya dawa. Matumizi ya anabolic steroids kwa ajili ya kuipa nguvu misuli yanaweza kusababisha korodani kusinyaa, na kupunguza uzalishaji wa mbegu. Matumizi ya cocaine na marijuana yanaweza kupunguza idadi na ubora wa mbegu.
Matumizi ya pombe na vinywaji vikali vya Caffein. Kunywa pombe knaweza kupunguza homoni ya testosterone na kupunguza uzalishaji wa mbegu.
Kazi. Baadhi ya kazi zinahusishwa na ugumba, zikiwemo uchomeleaji wa vyuma (welding), au zinazomtaka mtu kukaa kwa muda mrefu, kama kuendesha magari makubwa.
Uvutaji wa sigara. Watu wanaovuta sigara wanaweza kuwa na mbegu pungufu ukilinganisha na wale ambao hawavuti.
Msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo wa muda mrefu, na msongo kuhusu uwezo wa kuzalisha, unaaweza kuathiri uzalishwaji wa mbegu.
Unene. Unene unaweza kuathiri uwezo wa kuzalisha mbegu kwa namna nyingi.