Sababu za ongezeko kubwa la single maza

Hii changamoto ni duniani kote mimi nashauri tu wanawake wasizae na wanaume za watu bali wajikite kuanzisha mahusiano yatakayo kuwa bora kuliko changamoto za u single maza

Mtoto wa mama single maza anakosa vingi kutoka kwa baba kuliko kawaida.
 
Penye single maza kuna single faza walioshindwa kutimiza majukumu Yao
Hebu ongelea pia ongezeko la single faza sio kila siku kina maza tu
Hapa ndipo feminist mnapofeli mnalazimisha jinsia zote mbili zihukumumiwe kwa kigezo kimoja kitu ambacho hakiwezekani.

Leo mwanamke hata ukiwa masikini unajiona una haki ya kupendwa na mwanaume tena utaweka standard za juu kwa mwanaume unaemtaka lakini vipi mwanaume akiwa masikini? anaonekana useless asiye na haki ya kupendwa na mwanamke, hii ni kwa sababu hizi jinsia mbili zinahukumiwa kwa vigezo tofauti.

Ndivyo ilivyo kwenye single parent pia, haina shida kwenye profile ya mwanaume lakini kwenye profile ya mwanamke ni red flag kubwa sana
 
Kwanini nyie wanaume msizae na wanawake ambao wanawafaaa katika tabia ....mawazo ...mwenye uelewa kama wako ili tupunguze hili tatizo
 
Na wanaume wawajibike kwa watu wao waliowapa mimba asilaumiwe mmoja...BTW mimi sio feminist
 
Hiyo ni sahihi mkuu lakini vipi kuhusu wanaume wanaolaghai mabinti kihisia halafu wanawatelekeza baada ya mimba?
Tunatakiwa kuwa wakali kidogo kwenye mlezi ya mabinti zetu. Nakumbuka miaka iyo nasoma olevel ikigundulika binti kapewa mimba anafukuzwa nyumbani aende kwa aliempa iyo mimba, hukumu katili kama hizi zilisaidia sana kuwapa warning sign watoto wa kike.

Lakini leo hali ni tofauti mabinti na wanawake wana uhuru wa kufanya ngono hovyo hovyo bila kuwajibishwa na jamii wala familia. Tukirudisha ule ukali katika malezi itasaidia pia mabinti kuchukua tahadhari ivyo kutorubunika kirahisi.

Lakini kurusha lawama kwa wanaume wakati mabinti zetu tumewaachia uhuru wa kufanya ngono kiholela, kuvaa nusu uchi, kuonja onja hela za wanaume n.k basi wataendelea kupewa mimba na kutelekezwa tu.

Tuanze kwanza kuondoa huu uhuru wa kingono walipewa wanawake na kudhibiti hii advantage yao ya ushawishi wa kingono.
 
Na wanaume wawajibike kwa watu wao waliowapa mimba asilaumiwe mmoja...BTW mimi sio feminist
Shida ni kwamba mwanamke ndie anaekutana na izo consequences, hauwezi kusubiri kila upande uwajibishwe katika jambo ambalo wewe ni victim. Hapa hekima ni kujilinda kwanza wewe mwenyewe

Leo hii binti akipata mimba, atakachokifanya mwanaume ataikataa na kuendelea na maisha yake maana akikubali tu ni jela miaka 30. Lakini kwa huyu binti atasitisha masomo, atachafua profile yake, ataishi na chuki dhidi ya wanaume maisha yake yote. Unaweza kuaona hapo nani victim.

Sikubaliani na hao wanaowapa mimba wanawake na kuwatekeleza, vile vile sikubaliani na ubishi wa mwanamke wa kutaka kutunishiana msuli na mwanaume katika masuala ambayo mwanamke ni victim kwa sababu mwisho wa siku mwanamke ndie atakutana na consequences
 
Penye single maza kuna single faza walioshindwa kutimiza majukumu Yao
Hebu ongelea pia ongezeko la single faza sio kila siku kina maza tu
Lengo la mada, si kuwasimanga single maza, bali ni kutafuta suluhu ya changamoto hii mkuu.
 
Suluhu ianzie kwa wanaume wanaotelekeza hawa single maza
Hapana mkuu, tuanzie ktk malezi. Tukiwapa malezi bora binti zetu, na tukawafunza madhara ya kua single maza kabla ya ndoa, nadhani tunaweza punguza tatizo.
 
Hapana mkuu, tuanzie ktk malezi. Tukiwapa malezi bora binti zetu, na tukawafunza madhara ya kua single maza kabla ya ndoa, nadhani tunaweza punguza tatizo.
Sio binti tu hata vijana wa kiume wanastahili malezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…