Sababu za Pacome kutosafiri na timu Afrika Kusini

Sababu za Pacome kutosafiri na timu Afrika Kusini

Analog

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2024
Posts
323
Reaction score
618
BAADA ya sintofahamu ya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Pacome Zouzoua kutoongozana na kikosi cha timu hiyo kwenda Afrika Kusini, Tumezinyaka sababu ziliyomfanya asiwe sehemu ya kikosi hicho ni ishu ya pasipoti na amepewa siku tano kumaliza tatizo hilo kabla ya kuungana na wenzake Sauzi.

Awali kiungo huyo alikuwa pamoja na kikosi hicho tangu mazoezi hayo ya Pre Season kuanza, lakini juzi wakati timu uinaoondoka hakuwepo na ilishindikana kufahamika kwa mapema, hadi jana ilipoelezwa tatizo lililoomzuia asiondoke na wenzake ni pasipoti na amepewa siku tano kuanzia leo kuishughulikia.

“Sababu ya Pacome kutoondoka pamoja na wenzake ni pasipoti yake ilikuwa imejaa, hivyo inatakiwa arejee nchini kwao Ivory Coast kwaajili ya kupata kingine,” kilisema chanzo hicho kutoka Yanga na kuongeza;

“Kutokana na umuhimu wa sababu yake, uongozi umempa siku tano, ili akamilishe kila kitu, kisha ajiunge na wenzake Afrika Kusini, ambako watakaa wiki mbili na kurejea nchini kujiandaa na mambo mengine.”

Ndani ya hizo wiki mbili watakazokaa Afrika Kusini, Yanga itashiriki mashindano mawili ambayo ni Mpumalanga Cup na Toyota Cup, ikitarajiwa kuvaana ba timu za FC Augsburg ya Ujerumani na TS Galaxy kisha kumalizana na Kaizer Chiefs inayonolewa na kocha wa zamani wa klabu ya Yanga, Nasreddine Nabi.

Jeshi zima kwa asilimia 100 lipo Afrika Kusini.
 
Jeshi zima kwa asilimia 100 lipo Afrika Kusini.
Utasemaje jeshi zima kwa asilimia 100 lipo Afrika Kusini wakati mzee mwenye timu Magoma yupo zake Chanika, msemaji wenu yupo huku anabwabwaja hajui hata afanye kazi gani, na hapo hapo huyo mchezaji unayemuongelea naye hayupo huko. Sidhani kama asilimia 100 inafika asee
 
Back
Top Bottom