Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Je wajua kwanini unapoonyesha kumpenda sana na kumthamini sana mtu mwengine papohapo mwenzako huanza kuonyesha dharau kwako ,anakujibu vibaya kwa makusudi,anafanya makosa lakini haombi msamaha bali anataka uombe msamaha wewe,unajuwa kwanini kadiri unavyokuwa tegemezi ndivyo heshima yako inapungua kwa Watu wako wa karibu?
Unajua kwanini mtu mwengine akijua anapendwa sana huanza kuamini kwake hauna ujanja badala akupe heshima anakupuuza?
majibu ya maswali hayo yapo hapa chini
Watu wengine watakosa heshima kwako na kuanza kukuchulia poa kwa sababu zifuatazo
1.UPO NAO MUDA WOTE
Kama upo karibu sana na mtu yeyote,muda wowote anaweza kukupata endapo atahitaji kufanya hivyo,mtu huyo hawezi kuheshimu uwepo wako.
Unapokuwa unapatikana muda wote kwa mtu yeyote akihitaji uwepo wako husababisha unakosa umuhimu wowote katika maisha yake.
Kama kuna mtu muda wowote akipiga simu unapokea papo hapo,akituma sms unajibu papohapo hawezi kuheshimu uwepo wako katika maisha yake.
2.UNATEGEMEA SANA MAWAZO YAO KATIKA MAAMUZI YAKO
Mtu yeyote ambaye anajua huwezi kununua kitu chochote,kufanya maamuzi magumu bila kumshirikisha,mtu yeyote ambaye chochote ambacho unataka kufanya unakwenda kuomba ushauri wake hawezi kukuheshimu maishani mwake kwa sababu anakuona hujiwezi na hauna uwezo wa kuishi bila yeye.
3.WANAJUA UNAWAPENDA SANA
Mtu yeyote ambaye anajua kwa 100% unampenda sana kuliko watu wote duniani hawezi kukuheshimu maishani mwake.
Watu huwakosea heshima wenza wao , marafiki zao na ndugu zao pale ambapo wanakuwa na uhakika kwa 100% wanapendwa sana kuliko mtu yeyote.
Chunguza hata kwa watoto endapo mtoto akiwa na uhakika kwa 100% kwamba unampenda sana kuliko mtu yeyote hawezi kukuheshimu maishani mwake,kila siku utaishi kwa kutaka kumfurahisha na kumridhisha na siku zote mahitaji yake yanakuwa kipaumbele chako na mahitaji yako kwake yanakuwa kitu cha ziada.
4.UNANYENYEKEA KUPITA KIASI
Mtu yeyote ambaye anajua kwa 100% kwamba wewe unamnyenyekea sana hawezi kukuheshimu maishani mwake kwa sababu anajua unaishi kwa ajili ya kumridhisha yeye muda wote.
Angalia kwa marafiki zako ambao muda wote unaweza kuvunja ratiba zako kwa ajili yao tazama kama wao wanaweza kuvunja ratiba zao kwa ajili yako.
Tazama kwa watu wenye umri mkubwa sana kwako ambao unawaheshimu sana na huwa unakuwa mnyenyekevu sana mbele yao wakitaka kuzungumza na wewe hawajali chochote kuhusu ratiba zako,wakihitaji msaada wako hawataki kujua uwezo wako zaidi wanatoa agizo ila wewe ukiwa na shida kwao huwezi kutoa agizo badala yake unauliza ratiba zao,muda wao na vipaumbele vyao kwa sababu unaogopa watakasirika ila wao kwako hawana muda huo.
5.UNAOGOPA MIGOGORO NA UGOMVI
Mtu yeyote ambaye yupo na uhakika kwamba unaogopa kukwazana nae hawezi kukuheshimu maishani mwake kwa sababu anajua unaishi ili kumfurahisha na kumridhisha muda wote.
Kama kuna mtu yeyote ambaye huwa unatetemeka mbele yake kamwe hawezi kukuheshimu maishani mwake kwa sababu akiwa na hasira tu unaomba msamaha wewe hata kwa makosa yake.
6.UNAONA WAO NI WATU MUHIMU SANA MAISHANI MWAKO
Mtu yeyote ambaye kwako unaona ni mtu muhimu sana kuliko watu wote duniani kamwe hawezi kukuheshimu maishani mwake kwa sababu anajua huwezi kuishi bila yeye na kila kitu unafanya kwa ajili yake.
Tazama mtu ambaye unaamini kwamba bila yeye huwezi kupiga hatua fulani maishani mwako huwezi kuona anakupa umuhimu wowote.
Mtu yeyote ambaye furaha yake unaona ni muhimu sana kuliko furaha yako hawezi kukuheshimu maishani mwake wala hawezi kukuomba radhi akifanya makosa.
Kama upo tayari kutoa msaada muda wote hata kama hajaonyesha kuhitaji msaada wako kamwe hawezi kukuheshimu maishani mwake.
7.UNAJIONA MNYONGE SANA MBELE YAO
Kama unajiona mkosaji muda wote ukiwa na mtu yeyote Zingatia kwamba mtu huyo hawezi kukuheshimu maishani mwake kwa sababu akiwa na hasira unahisi umefanya makosa wewe na akiwa na furaha unahisi ni kwa sababu ya kile ambacho unamfanyia .
Zingatia kwamba watu wote duniani wapo na makosa, mapungufu,siri nzito zenye fedheha ambazo hawana uwezo wa kusimulia kwa kila mtu.
Ukizingatia hilo itakuwa rahisi kuacha kujilaumu kupita kiasi kama hauna maelewano mazuri na mtu yeyote.
Ufumbuzi wake ni kugeuza sababu za watu kukukosea heshima badala yake weka mipaka, tambua tabia gani huwezi kuvumilia kutoka kwa watu wengine,acha kuwapa watu wengine umuhimu mkubwa sana kuliko uhalisia wake, fahamu njia za kukabiliana na migogoro katika mahusiano yako.