Sababu zilizopelekea mke wa bilionea Msuya kushinda kesi ya mauji ya Aneth Msuya (wifi yake )

Sababu zilizopelekea mke wa bilionea Msuya kushinda kesi ya mauji ya Aneth Msuya (wifi yake )

mwakani naolewa

Senior Member
Joined
Jul 25, 2024
Posts
148
Reaction score
426
Moja kati ya hoja zilizomfanya Mke wa Marehemu bilionea Msuya ashinde kesi ya mauaji ya wifi yake ni upande wa mashtaka kuwa na pungufu ya kushindwa kufuata kanuni za kumhoji mshtakiwa pia na kukosa ushahidi wa dhahiri wa watuhumiwa hao kuwepo eneo la tukio au karibu na eneo la tukio.

Ushahidi wa kusema kwamba Miriam alimuua wifi yake kwasababu ya mgogoro wa mirathi Mshtakiwa alilipinga kizimbani kwa kusema kwamba aliwapa wifi zake wote milioni sabini za kitanzania kila mmoja pia asingeweza kumuua wifi yake kwasababu ni kama mtoto wake alimlea yeye na marehemu mume wake kama mtoto wao .

Pia katika ushahidi wa video ya mtuhumiwa kukiri mauaji haikuweza kuletwa mahakamani kutokana na kushindwa kufuata kanuni za mahojiano na mtuhumiwa 🥲.

Na zaidi mtuhumiwa alisema kwamba aliteswa sana ili akiri kuwa anahusika na kifo cha wifi yake na mengine mengi tu.

Je ushahidi huu ni kigezo cha kufanya mtuhumiwa kushinda kesi

Pia soma

- Mjane wa bilionea Msuya aachiwa huru, Mahakama haijamkuta na hatia mauaji ya Aneth Msuya
 
Back
Top Bottom