Sababu zinazopelekea kuongezeka kwa vitendo vya ukatili kwa watoto katika jamii

Sababu zinazopelekea kuongezeka kwa vitendo vya ukatili kwa watoto katika jamii

Baba ilumba

Member
Joined
Apr 18, 2020
Posts
37
Reaction score
49
Kwa miaka ya hivi karibuni jamii imekuwa ikishuhudia vitendo vingi ambavyo kwa namna moja ama nyingine si vya kingwana kabisa hasa kwa watoto wadogo waliopo chini ya umri wa miaka 15.

Sababu zimekuwa nyingi mno zinazopelekea kwa vitendo hivi kuwepo na kuongezeka kwa kasi sana baadhi ya sababu hizo ni pamoja na ;

1.Imani potofu .
2.Utandawazi.
3.Wivu ama migogoro baina ya wazazi .
4.Kukosekana kwa utu n.k

Baadhi ya vitendo hivyo ni pamoja na;
1.Utumikiswaji wa watoto katika ajira bubu na katika mazingira hatari.
2.Unyanyasaji wa kijinsia /kingono hapa nazani tumisikia wababa wanawaingilia kingono hadi watoto wa miaka 4.
3.Kuteswa sana hasa na wazazi wa kambo .
4.Kunyimwa haki za msingi kama watoto n.k.

Licha ya serikali na taasisi nyingi kukesha wakipinga vitendo hivi lakini hali inaonekana kuwa ileile kila kuchwapo.

TUJUZANE[/|]
1.Ni kipi hasa kinapelekea vitendo hivi kuongezeka kwa kasi sana na pia nini kifanyike kupunguza ama kutokomeza kabisa matendo haya maovu katika jamii.
 
Mm bado sijapata booklet tichaaaaaa
Reading before answer the question above
 
Bado mtoa mada hujaweka wazi unaongelea ukatili gani hasa, huu uzi mzuri ila uwasilishaji ni katili kwa wachangiaji, jaribu kuuweka sawa.

NB. Ni mzuri na utaelimisha watu pia.
 
Back
Top Bottom