Sababu zipi zilikupelekea ukawa shabiki wa hiyo timu yako ya sasa pale Uingereza?

bolivia

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2021
Posts
3,083
Reaction score
5,179
Mimi ni shabiki wa Liverpool kindaki kindaki siyo masihara,

Sababu iliyopelekea kuipenda hii ni;

1. Bwana mdogo Michael Owen, enzi hizo vile alivyo kasi na ufungaji wake na falsafa za pale kwenye timu ambazo zilianzishwa na Bill Shanks, moja kati wa wachezaji hatari kuwahi kutokea hapo na baadae kuwa mwalim. Falsafa ya kucheza kama upo kwenye fainali.

2. Tukio la pili ni ule usiku wa UEFA Champions League dhidi ya AC Milan ya enzi zile kwa kupiga ile come back ya hatari zaidi Duniani. Hii ilipelekea mimi kuwa shabiki mzuri wa Liverpool. Huu uzi utunzwe nina imani kuna siku nitakanyaga uwanja wa Anfield kwa uwezo wa Mungu.

Tukio lipi lilikupelekea kushabikia hiyo timu yako?

#TheReds
 
Nwanko Kanu alinipeleka Arsenal enzi za JVC.mzee Wenger kipindi icho anasajili vototo mwanzo mwisho.
 
Kama ujuavyo wabongo wengi tunavutiwa na maniga wanaokipiga ulaya, mie bana world cup 2002, nilikuwa bega kwa bega na Senegal wakiwa na star wao mtukutu ostaz el haji diof, nilvutiwa na jinsi walivomtoa nishai bingwa mtetezi, sasa Liverpool walivomsaini yule kiboko ya wazungu basi tangu siku ile nikawa nimechanjiwa damu ya hao kuku wa anfield.
 
Una maoni gani baada ya leo kubanduliwa kimoja cha kitia mimba
 
Karibu kwenye chama bro
 
Captain Lucas Radebe na Jimmy floyd Haselbaink walisababisha niipende Leeds United enzi hizo wanakimbiza kwelikweli. Ila kwa sasa hivi huniambii kitu kwa Gunners
Leeds united mkuu, aah aah umetisha wewe
 
Arsenal 2003/4 kisa ile unbeaten hahaaa
Nilikuwa dogoless kipindi iko
 
Thierry Henry, Sylvan Wiltord, Denise Berkamp, Djumberg,,, acha tu
 
Mimi manunited fun since 1999 SABABU kilikuwa kikosi Bora Hadi Leo nimshabiki kindaki ndaki wa timu iyo
 
Nilikuwa napiga sana kazi chafu nikiwa ground enzi hizo na nilikuwa nawaangalia sana Gilberto Silva na Patrick Vieira basi ndio ukawa mwanzo wa kuipenda arsenal hasa lile bato la Roy wa nyumbu na Patrick
 
Nilikuwa fan wa real madrid kwasababu ya akina Zidane (maana mimi huwa naipenda France kwenye world cup tangu 98). Ila nilikuwa naipenda arsenal kwasababu ya Thierry Henry.

Sasa mwaka 2006 ndio nikagundua naipenda zaidi arsenal maana walikutana kwenye ucl na nilikuwa naishabikia arsenal against madrid siku ile na kama kawaida ya Henry, madrid alikufa kwa aggregate ya 1 bila.

Ila sasa cha kushangaza nikaja kuwa fan wa barcelona na kuichukia madrid mpaka leo baada ya wao kumchukua Christiano Ronaldo na Barcelona wakamchukua Henry. Siku hizi barca siwapendi tena baada ya Messi kuondoka.

Ila ni die hard fan wa Arsenal, epl, fa na europa champions 2022/23.
 
Nilikuwa napiga sana kazi chafu nikiwa ground enzi hizo na nilikuwa nawaangalia sana Gilberto Silva na Patrick Vieira basi ndio ukawa mwanzo wa kuipenda arsenal hasa lile bato la Roy wa nyumbu na Patrick
SABABU ni hiyo tulishinda teble makombe yote magumu ulaya kipindi hiko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…