Hapo kwenye namba mbili hapo, nimekumbuka habari niliyoipata leo asubuhi kutoka kwa rafiki yangu.<br />
Ni hivi leo asubuhi rafiki yangu(best friend/family friend) anayeishi kw muda nje ya nchi amenipigia simu akilalamika kuhusu tabia ya Gf wake. Anasema amekuwa akimtumia pesa nyingi tu kwa ajili ya matumizi na vitu kama hivyo, akanipa mfano mwezi machi mwaka huu alimtumia sh.laki saba(700,000) kwa ajili ya kulipia kodi ya nyumba ya huyo GF wake, ikafika mwisho wa april binti akamwambia jamaa anashida sana na sh.laki nne,jamaa bila kuchelewa akamtumia haraka. Sasa wiki iliyopita ijumaa, binti kamwomba jamaa sh.laki tano. Jamaa akamjibu tu kistaarabu kuwa kwa sasa hana hiyo hela kwa sababu ni muda si mrefu ametuma hela kwa ajili ya kumplipia ada ya chuo ya mdogo wake, hivyo kwa kipindi hiki hana hiyo hela. Anasema baada ya kumjibu hivyo binti,mawasiliano yamekuwa dry. Namaanisha toka siku ya ijumaa mawasiliano yao sio mazuri kama zamani,jamaa akipiga binti anamjibu kama hataki,akituma msg hajibu kabisa jamaa akiuliza mbona hunijibu dada anasema hajapata msg yoyote.<br />
Jamaa anasema kwa sasa anamuangalia tu aone mwisho wake, kwa hatua waliyokuwepo ni zaidi ya uchumba kwani ndoa wanategemea kuwa mwisho wa mwaka huu au mwanzoni mwa next year. Concern ya jamaa ni kuwa kama huyo dada ameanza tabia hii akiwa hata bado ndoa je akimuoa na siku akamwambia sina hela si atakimbiwa?<br />
Nimemshauri aongee naye kwa kirefu na amwambie kuhusu hiyo tabia, amekubali hilo ila amesema akimjibuw vibaya chochote kinaweza tokea.