Sabasaba 2020: Wizara ya Kilimo na Uvuvi na samaki aina ya Silikanti

chuma_cha_pua

Member
Joined
Sep 28, 2013
Posts
24
Reaction score
12
Habari wanajamvi,

Kuna jambo nimeona la kushangaza kidogo katika maonyesho haya ya sabasaba katika banda la Wizara ya Kilimo na Uvuvi, kuna sanamu ya huyu samaki anayeitwa coelacanth au silikanti ambaye ni aina ya samaki anayezaa badala ya kutaga mayai, na pia inasemekana ni jamii ya samaki aliyeishi kipindi kile cha wanyama waliojulikana kama Dinasours.

Cha kushangaza ni kwamba hawa samaki ni samaki ambao wapo huku kwetu Tanzania kutokana na maelezo yaliyokuwa yanatolewa na afisa aliyekuwepo katika hilo banda, ila kwanini Katika maonyesho kama haya ambayo ni makubwa kwa nchi yetu kusikuwepo na huyu samaki ambaye ni hai na sio sanamu?

Je, Wizara haioni umuhimu wa kumtafuta huyu samaki na kuwa naye kwa ajili ya utalii na maonyesho kama haya.

09f8be492a470304353ca4b8d774df65.jpg
 
Aina hiyo ya samaki wapo wengi pwani ya bahari ya Hindi wanaishi kwenye kina kirefu cha maji,hiyo sanamu tu tayari ni utalii tosha.
 
Walishaonekana Kunduchi kwa wingi....extinct kwa Beberu, huku wapo.

Everyday is Saturday............................ 😎
 
Habari wanajamvi,

Kuna jambo nimeona la kushangaza kidogo katika maonyesho haya ya sabasaba katika banda la Wizara ya Kilimo na Uvuvi, kuna sanamu ya huyu samaki anayeitwa coelacanth au silikanti ambaye ni aina ya samaki anayezaa badala ya kutaga mayai, na pia inasemekana ni jamii ya samaki aliyeishi kipindi kile cha wanyama waliojulikana kama Dinasours.

Cha kushangaza ni kwamba hawa samaki ni samaki ambao wapo huku kwetu Tanzania kutokana na maelezo yaliyokuwa yanatolewa na afisa aliyekuwepo katika hilo banda, ila kwanini Katika maonyesho kama haya ambayo ni makubwa kwa nchi yetu kusikuwepo na huyu samaki ambaye ni hai na sio sanamu?

Je, Wizara haioni umuhimu wa kumtafuta huyu samaki na kuwa naye kwa ajili ya utalii na maonyesho kama haya.

View attachment 1500094
 
Back
Top Bottom