Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,835
- 23,776
*
HUKUMU YA SABAYA
Tumefikaje Hapa?
Ilikuwaje? Kipi hakikufanya kazi yake sawasawa? Taifa lenye mihimili yote, taasisi mbalimbali, vyombo vya habari, vyombo vya ulinzi na jumuia za kimataifa, likaacha mtu mmoja akateka, akaiba, akatesa, akabaka, na kuvunja sheria zote?
Kabla ya kuteuliwa kuwa DC, Sabaya alikuwa chini ya uchunguzi wa Polisi kwa makosa ya kutapeli na kujifanya Afisa wa "Chombo" nyeti.
Ndani ya "chombo" nyeti ni kosa la ahera kutumia kitambulisho cha "chombo" kujipatia huduma au kutisha watu. Ni kosa kubwa zaidi "kujifanya" na "kughushi" kitambulisho cha chombo.
Kabla Polisi hawajampeleka mahakamani, akateuliwa kuwa DC.
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya (Sasa Mbunge) alitia mkono kwenye mamlaka ya uteuzi mpaka Sabaya akateuliwa.
Lilikuwa kosa kubwa. Linaigharimu serikali, linaichafua mamlaka ya uteuzi.
Utetezi wa Sabaya katika kesi hii kuwa alitumwa na mamlaka ya uteuzi ni mbaya sana. Unaichafua taasisi ya uteuzi, unakichafua "chombo" nyeti na kudhalilisha viapo. Mteuzi na Mteuliwa Hawakufundwa. Tunabaki kujiuliza:
I) Kwa hiyo mamlaka ya uteuzi iliagiza Sabaya aibe, abake, apore, aue, atese, ateke na kughushi?
Ii) Kwa hiyo mamlaka ya uteuzi imehukumiwa kama mshirika wa jinai hizi?
III) Kwa hiyo kama si Kinga, tungetumia "subpoena" kuiita mamlaka ya uteuzi kizimbani kujieleza?
iv) Kwa hiyo tungekuwa na utawala mzuri wa sheria, bunge lingeteua Kamati Maalum ya kibunge kuchunguza makosa haya makubwa yaliyotendwa na mamlaka ya uteuzi?(Watergate).
v) Kwa hiyo Sabaya ameivua nguo mamlaka ya uteuzi kwa madai haya mazito akiwa mbele ya kiapo au amedanganya chini ya kiapo?
Madai ya Katiba Mpya yanaonekana wazi. Katika kesi hii, mambo mapya ya kuzingatiwa katika katika mpya yamejitokeza:
1. Nafasi ya DC na RC: Wateuliwe au wachaguliwe? Je ni wanahitajika ikiwa tuna dhamira ya kuimarisha serikali za mitaa?
2. Kinga ya Rais: iwepo au isiwepo? Ikinge yapi na kuacha yapi? Ianze lini na kukoma lini?
3. Wateule kupitiwa na Kamati fulani kabla ya kuthibitishwa
4. Njia ya kushughulikia mamlaka kuu endapo zimekiuka katiba
5. Namna ya kushughulika na wateule wenye viapo endapo wanashtakiwa katika mahakama za wazi.
6. Usawa mbele ya sheria.
Uhuru "Chombo" imehojiwa na Kesi hii. Kimepoteza uhuru na weredi. Tufanye Nini?
Je kama Taifa twaweza kuungana, tukasahau tofauti zetu na kutamka kwa pamoja kuwa "ISITOKEE TENA"?
Bag-Onza