Sabaya na Manabii wa Mola tusio Wakubali

Sabaya na Manabii wa Mola tusio Wakubali

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Haya si maneno yangu:

"Nabii hakubaliki kwao."

Nini kulikuwa kigeni kwake aliyekuwa Mh. Sabaya? Je hakuonywa? Au alitegemea manabii waje na mbawa zao kama malaika straight toka kwa Mola?



Ikumbukwe mheshimiwa Lema aliwahi toa maonyo si kwa ndugu huyu pekee, na kweli yakatokea.



Ama kweli majuto ni mjukuu.
 
Nenda sabaya wasalimu uendako🖐️🖐️🖐️
 
Kwa kweli itabidi kuwe fair...Mbowe naye akila 30 watu wawe watulivu.....

Kwa kosa lipi mjomba? Hukumu ya Sabaya Kwa ufupi iko humu:

1. Imethibitika kuwa Sabaya alikuwa na silaha kwenye duka walilolivamia kinyume cha sheria.
2. Imethibitika Sabaya akiwa ndani ya duka na silaha, wenziwe wawili walikuwa nje ya duka wakiwa na silaha kinyume cha sheria.
3. Sabaya na wenzake walichukua udhibiti wa duka la shahidi kwa kutumia silaha kinyume cha sheria.
4. Hakuna shaka kuwa duka la shahidi lilivamiwa na washitakiwa wakiwa na silaha kinyume cha sheria.

Humo ndimo mvua 30 zinavyo dadavuliwa hatimaye.

Kama ni Kingai na wenzake, tuko hapa:

Hoja za Mawakili wa Serikali dhidi ya Adamoo

Tunasubiri udadavuzi wa Mh Jaji.

Yetu ni subira.
 
Na siku Mbowe akila mvua uje ushangilie hivyohivyo
Sio kila anayeshangilia kufungwa kwa Sabaya ni CHADEMA Mateso na Uonevu wa Sabaya kila mwenye HOFU ya MUNGU Lazima ASHANGILIE ni SHETANI TU kama WEWE ndio unaumia Nakipongeza Chama langu CCM kwa kumfunga Mhuni Sabaya
 
Ndivyo maana hata leo miaka 2000 baadaye unasema alionewa.

Swali la msingi, Sabaya kaonewa?
Sabaya hajaonewa hata kipofu anajua hilo,kwa kesi ya Mbowe kuna uonevu mkubwa sana unaohusu siasa baina ya ccm na Chadema.Kosa la Mbowe ni kuwa na msimamo thabiti ambao unawafanya ccm wasijiamini,hivyo kutumia nguvu ya dola ili kumwangamiza Mbowe kisiasa.
 
Sabaya hajaonewa hata kipofu anajua hilo,kwa kesi ya Mbowe kuna uonevu mkubwa sana unaohusu siasa baina ya ccm na Chadema.Kosa la Mbowe ni kuwa na msimamo thabiti ambao unawafanya ccm wasijiamini,hivyo kutumia nguvu ya dola ili kumwangamiza Mbowe kisiasa.

Iko namna hii. Kesi ni mahala pa wazi.

Mahakama inawajibu wa kuonyesha kuwa inatenda haki.

Ni vyema kuwa unatambua pasi na shaka kuwa Sabaya hajaonewa.

Tafakari nini kingetokea kama angeshinda kesi?
 
Back
Top Bottom