Idadi ya chini ya kuanzisha SACCOS ni Wanachama 20,eneo mnaloanzisha liwe na uwezekano wa wanachama wengine kujiunga nanyi wenye nia inayofanana na waanzilishi.Kuwe na Mfungamano( kitu kinachowaunganisha). SACCOS mnayotarajia kuianzisha iwe inaweza kujiendesha kiuchumi.
Kwa maelekezo sahihi na kamili wasiliana na Afisa Ushirika wa Wilaya yako. Kila Halmashauri Tanzania Bara ina Afisa Ushirika .
Huwezi kuanzisha SACCOS /Chama chochote cha Ushirika bila Afisa Ushirika wa Wilaya husika kushirikishwa.Ndiye Mwenyekiti wa Mkutano anzilishi unaunda Bodi anzilishi na kuwashauri namna ya kuandaa masharti ya SACCOS/Chama chenu. Ndiye atakayewaelekeza kwa Mrajis Msaidizi/Mrajis wa Vyama vya Ushirika. SACCOS ni mojawapo ya aina za Vyama vya Ushirika,Vyama vyote vya Ushirika havisajiliwi BTRELA wala mambo ya ndani.