"Sadaka ya kumuona nabii ni utapeli mtupu"- Pastor Wambura Magesa

"Sadaka ya kumuona nabii ni utapeli mtupu"- Pastor Wambura Magesa

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
1,497
Reaction score
2,681
"Wenye shida waliwaona manabii,mitume na Yesu Kristo mwenyewe,bila kulipia fedha inayoitwa sadaka.Na matatizo yao yalitatuliwa bila gharama yoyote.

Siyo agizo la Mungu wala mapenzi yake kuwaona watumishi wake;eti mpaka wenye matatizo na magonjwa walipie kiasi fulani cha fedha,ambacho kimewekwa na kiwango maalumu kabisa.Hawa mitume na manabii wenu wanaotoza watu pesa za kuwaona ni wachawi.Wana sadaka kibao ambazo ni utapeli mtupu.Sadaka za kitapeli ni pamoja na sadaka ya ukombozi,sadaka ya mzaliwa wa kwanza,sadaka ya kujilipua, sadaka ya kujimaliza, sadaka ya kujiunganisha na madhabahu.Sadaka hizi hazipo kwenye agano jipya,ambalo ndilo agano la kanisa.

Bado hawatosheki wanawauzia watu vitu vya upako kama maji,chumvi,udongo,kalamu,kokoto,shanga,mafuta,picha,nk.Wanafanya miujiza na kutoa unabii kichawi,japo wanalitaja jina la Yesu Kristo.Ukweli ni kuwa wauza vitu vya upako wote duniani ni wachawi.Mtume Petro alimkemea Simoni mchawi aliyetaka kutoa fedha kwa ajili ya vipawa vya Roho Mtakatifu.Kwani vipawa na karama za Roho Mtakatifu huwezi kamwe kuvilipia.Gharama yake ni damu ya Yesu Kristo pekee.

Soma { matendo 8:20-21, Lakini Petro akamwambia,Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe,kwa kuwa umedhania ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali.Huna fungu wala huna sehemu ktk jambo hili,kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu}.

Ole wenu vipofu mnaotafuta miujiza, ishara na unabii na hamtaki kweli ya Neno la Mungu.Wengi mmeishia kuunganishwa na miungu ya wachawi wanaojiita mitume na manabii.Mnatumikia roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani.Siku ya hukumu patakuwa hapatoshi.

Nimetumwa kunyoosha rula kwenye mwili wa Kristo.Nazifungua akili na fikra zilizofungwa na wachawi,wajifanyao ni watumishi wa Mungu"

PASTOR WAMBURA MAGESA.

Tuandikie Maoni yako hapa chini 👇

#AtumediaOnlineTv
#AtumediaUpdates
#GospelToTheWorld
#SisiNdioWaleTunaosaidiwaNaBwana
 
Pana watumishi wa Mungu Pana menta pana motivation speaker japo wote wamejifichia kwenye utumishi wa Mungu.
 
Kanisa ni moja tu Katoliki la Kristo makanisa haya ya kiroho yamekuja kuuharibu Ukristo uonekane no tofauti na upagani kwa kuingiza mambo ya kidunia makanisa kupitia manyimbo yasiyo na uvuvio kwa densi za kuzimu mfano mastep ya mashetani, wanawake kukaa uchi makanisani ili kuchochea zinaaa.
Mafundisho mepesi
 
Unakimbia sadaka na michango kwenye jumuia unakwenda kutana na michango kibao kwa hizi ministry za mke na mume
 
Mama shangazi Dada zetu ni nini haiingii akilini kuwa hawa ni matapeli?

Kama wana uwezo wa kuponya sijui kutabiri waende mahospitalini wakawaponye huko!

Tunaangamia kwa kukosa maarifa!

Aliyewaloga Wanawake sijui ni nani?
 
biashara imehamia makanisani sikuhz utapeli, wanashindana zimekua taasisi
 
Back
Top Bottom