Salaam, Shalom!!!
Kuna wajinga wengi wanaodhani kuwa watumishi wa Mungu na Mungu mkuu kuwa Wana njaa na kudhani kuwa wapo Ili kukusanya sadaka Ili kujiongezea ukwasi,
Usilolijua ni kuwa, SADAKA HUKATALIWA, Fuatana nami.
1. Nabii Elisha, anakataa vitofali sitini vya Dhahabu alivyoleta Naamani, Jemedari wa Jeshi la nchi ya Shamu aliyekuwa na ukoma, sadaka aliyobeba ilibeba ukoma na ilitokana na miungu iliyokuwa kinyume na Mungu wa Nabii Elisha, Mungu mkuu akamkataza Nabii Elisha asipokee sadaka hiyo, amponye Bure bila kupokea chochote Toka kwake, Mtumishi wa Elisha aliingiwa na tamaa, akatangulia mbele na kwenda kupokea sadaka hiyo Kwa Hila, matokeo ni kuwa, Ukoma alioponywa Naamani, ulimrudia mtumishi wa Elisha.
2. Yuda anapokea vipande 30 vya Fedha na kumsaliti Yesu, Yesu akakamatwa na kusulubiwa, Yuda anaamua kuzichukua sadaka na kuipeleka Kwa waliomuhonga wanaokataa, anaamua kuipeleka madhabahuni napo inakataliwa, sadaka hiyo inampelekea kwenda kujinyonga. Sadaka hiyo ilibeba LAANA hivyo HAIPOKELEWI.
3. Kaini anatoa sadaka iliyobeba uharibifu na UOVU Toka ndani ya moyo wake, sadaka Mungu anaikataa, Kaini anaamua kwenda kuua baada ya sadaka yake kukataliwa, ndipo ujue sadaka iliyotokana na UOVU, ukipeleka madhabahuni, itakurudia kukumaliza.
4. Hanania na mkewe, Saphira, wanakubaliana kuuza shamba Ili wapate pesa ya Kutoa sadaka Yao, tamaa inawaingia baada ya kupata pesa, wanaamua kupunguza kiasi Kisha wanapeleka sadaka pungufu kinyume na nadhiri Yao. Ingekuwa Leo wachungaji Hawa wasingejua Hila hiyo, lakini Petro Kwa msaada wa Roho MTAKATIFU anajua na kuikataa sadaka hiyo, matokeo ya kukataliwa sadaka hiyo, mume na mke, wanafia madhabahuni na wanapelekwa kuzikwa, matokeo ni kukataliwa sadaka ya uharibifu.
5. Yesu pia alikataa kupokea sadaka ya Zakayo mtoza ushuru, baada ya kukutana na neema ya Kristo, akaazimia Kutoa nusu ya Mali yake Kwa maskini, na hatuoni popote Yesu akipokea chochote Toka Kwa Zakayo maana pesa zake alizopata akiwa TRA ya Israeli wakati huo, ilitokana na RUSHWA na kupiga madeal na dhuluma, pesa hizo zinatakiwa zirudishwe Kwa maskini na wajane na yatima waliodhulumiwa pesa hizo indirectly, na ndiko Zakayo alikozielekeza sadaka hizo Kwa msaada wa Roho mtakatifu, na Si kuzipeleka madhabahuni,Kanisani.
FUNZO.
1. Ewe kahaba, ukilipwa pesa Kutoka KAZI haramu ya kujiuza, hiyo ni "sadaka ya mbwa" HAIPOKELEWI Kanisani, katika madhabahu takatifu, ukiitoa, unaharakisha MAUTI Yako. Anza kwanza kuacha ukahaba, fanya KAZI halali ,malipo halali ndiyo uyatolee sadaka.
2. Wewe muuaji, umeua mtu Kwa kulipwa, unaona upeleke sehemu ya sadaka hiyo ya Damu madhabahuni, Kanisani, ukidhani utamhonga Mungu akusamehe dhambi,jua kuwa haitapokelewa, na sadaka hiyo itageuka kuwa moto kichwani mwako, hutopata utulivu, tubu kwanza, acha uuaji, fanya KAZI halali ndipo peleka sadaka hiyo madhabahuni.
3. Umeiba pesa za Umma, umetapeli mtu, umepokea RUSHWA, Kisha unachukua sehemu ya pesa hiyo ya wizi na kuipeleka madhabahuni Kanisani, wachungaji na maaskofu na mapadri wa Leo, hawataki kusikia huduma ya unabii ndani ya Kanisa sababu, manabii ndani ya Kanisa wangeona na kuwatimua wezi wasilete sadaka ovu ndani ya Kanisa. Kutoruhusu manabii makanisani ndio chanzo Cha wezi kuleta RUSHWA Kanisani Kisha wanapigiwa makofi Badala ya kutimuliwa kama alivyofanya Elisha kumtimua Naamani asikabidhi Dhahabu Ile madhabahu ya Mungu Mkuu.
4. Unauza au unamiliki bar, unauza pombe, Kisha unachukua sehemu ya mapato yatokanayo na pombe unapeleka Kanisani, yaani unamwambia Mungu Asante Kwa kukusaidia kupata walevi wengi wa kununua pombe Ili ulete sadaka Kanisani, unajidanganya, sadaka hiyo HAIPOKELEWI, itazidisha matatizo kwako na Kwa familia Yako. Acha KAZI hiyo, fanya KAZI halali, Kisha toa sadaka na ZAKA, ubarikiwe.
5. Una chuki na ugomvi na ndugu Yako au Jirani Yako, au mke wako, usipende Kutoa sadaka madhabahuni kabla hujasameheana nao au kumaliza magomvi na tofauti hizo, usiposuluhisha, sadaka Yako itageuka kuwa LAANA na kukuharibia maisha Yako. Ni muhimu sana kuzingatia nisemacho, maana wengi wanatoa sadaka na ZAKA na wanarudi nyuma kiuchumi, kimahusiabo, Kijamii nk nk bila kujua sadaka walizotoa bila TOBA ndio chanzo.
HITIMISHO:
Ikiwa hujampa Yesu maisha Yako na ulikuwa ukitoa sadaka iliyotokana na wizi au dhambi madhabahuni na watumishi wasio na macho ya kiroho wanaipokea na kukuombea baraka fake, kumbe unalaanika na kurudi nyumbani na LAANA Badala ya baraka, unajikuta matatizo yanazidi Badala ya kupungua, fuatisha Sala hii:
EE MUNGU KATIKA JINA LA YESU KRISTO, NINAKUKIRI WEWE KUWA BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU, ULIANDIKE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA UZIMA, NIPE UWEZO WA KUISHI MAISHA MATAKATIFU, DHAMBI ISINISHINDE, UOVU USINISHINDE, NINAOMBA HAYO KUPITIA JINA LA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YANGU. AAMEN.
Mungu awapendaye sana, Awabariki.
Source : 1. (2 Kings, chapter 5:1.....),
(Mwanzo 4:1-12), (Mathayo 27:3....)
Karibuni 🙏