hivi sisi watz tunafaidi wapi kati ya EAC na sadc? wapi kwenye faida zaidi kati ya pande zetu hizi mbili?
Inawezekana kote kukawa na faida, kwa maoni yangu. EAC, COMESA na SADC zote ni njia kuu za kuifanya Afrika ije kuwa chini ya ya muungano mmoja siku za baadaye. Kwa hiyo kila walalofanya, wanafocus Africa intergration bid.
Lakini udhaifu wa Tanzania kuwa EAC ni kuwa kwenye nchi nyingi zilizoko COMESA, na ambazo hazitaki kuheshimu uhuru wa Tanzania kuwa SADC. Kwa sababu zenyewe ziko COMESA, basi zinai bully Tanzania nayo iwe COMESA.
Pia, in terms of trading, Tanzania imekuwa zaidi ni soko la Kenya ambayo private sector ilianza siku nyingi, hivyo kutufanya tuwe koloni la Kenya kiuchumi. Kenya ina tatizo la kuwa dishonest inapokuwa kwenye maslahi, na hili linatokana na ukweli kuwa ina nguvu za kuichumi kuliko jirani zake. Kama kungekuwa na nchi nyingi zaidi kwenye block hii ambazo ama zingekuwa na nguvu au dhaifu, zingesaidia kuneutralize msimamo huu wa Kenya.
Unapopima mafaniko ya EAC, kumbuka pia kuwa kuna focus ya federation. Politically, nchi zote hizi zinatofautiana sana namna ya kutatua political upsets. Of all, Tanzania pamoja na matatizo yake, ndo the most stable one, na wananchi wake wana muundo wa ajabu wa kutatua matatizo yao.
Hii ina maana kuwa Over ambitions za watu kama Museveni inapokuja suala la urais wa EAC, na namna tatizo la akina Kony, tribalism kwenye politics both Uganda na Kenya, vinawaput off wengi wetu katika EAC.
Nikipata wasaa mzuri zaidi nitatafuta takwimu zinazofaa. Bado nadhani sijajiubu swali lako sawa sawa, lakini SADC ilianza kwa political thrust wakati ule ikiwa SADCC, na baadaye ikashift. SADC, kwa kuwa ina member wengi, maamuzi yake yamekuwa thabiti, japo nayo huwa inachemsha sehemu fulani. South Africa huwa inatoa mchango mkubwa kwenye SADC kwa kuwa inataka iwe zaidi ya rival wake COMESA. Na hii ni healthy situation.
Binafsi naona EAC kama utapeli mwingi, huku kila mtu akitolea macho resources za Tanzania. Kumbuka hata namna wazo la kuanzisha EAC lilivyochemshwa: from Up to bottom, badala ya bottom up. Ndo maana kwenye survey ya watu wanaotaka ku fast track federation, imeshindikana.