kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Ugeni wa SADC ni wetu sote na tunaupenda sana Sisi Watanzania, lakini kamati ya mapokezi fanyeni kila kitu kinachowezekana ili msisababishe foleni ndefu za muda mrefu njiani Kwa wananchi wenzenu wanaotumia barabara hizo. Tuache viongozi hawa washuke na waondoka haraka airport bila ya kuwachelewesha Kwa maonyesho ya vikundi ili kupunguza muda wa wananchi kusubiri kwenye foleni. Na njia mojawapo ya kupunguza foleni ni kupunguza kuwasubirisha viongozi hao wanapofika airport Kwa kuwaonyesha ngoma, sarakasi, nyimbo na mbwembwe nyingi nyingine. Ndiyo maana katika nchi nyingine inakofanyikia mikutano kama hiyo hakuna vitu kama hivyo(entertainment) kwa kuhofia kuwasumbua watu wao barabarani wanaotumia barabara wanazopita viongozi. Foleni inaanzia tazara hadi kimara mwisho bwana!
Hasara ya watu kukaa kwenye foleni Kwa muda mrefu ni kubwa sana na wakati mwingine inagharimu maisha ya watu.
Natoa hoja.
Hasara ya watu kukaa kwenye foleni Kwa muda mrefu ni kubwa sana na wakati mwingine inagharimu maisha ya watu.
Natoa hoja.