SoC03 Safari maridadi juu ya mafanikio

SoC03 Safari maridadi juu ya mafanikio

Stories of Change - 2023 Competition

My beginning

Member
Joined
May 31, 2023
Posts
11
Reaction score
8
Katika maisha Kila binadamu anaye hitaji kufanikiwa katika jambo, lengo au ndoto fulani ni lazima awe na sifa au tabia fulani katika kufanikisha jambo au lengo Hilo, na hii ndio tunaita safari maridadi juu ya mafanikio. Watu wengi walioweza kufanikiwa huwa na tabia fulani kwenye maisha Yao ndiyo maana hufanikiwa Kila mara wanapofanya jambo au kitu fulani.

Mtafiti wa mambo ya mafanikio Ftomas Corley aliweza kutumia Miaka mitano kuchunguza maisha ya Kila siku ya matarajiri na maskini na kugundua kuwa kitu kimojawapo wanachotofautiana sana ni tabia zao na mambo wanayofanya Kila siku. Vile vile mfukunzi wa mambo ya uongozi na mfanyabiashara Mike Murdock aliwahi kusema kuwa "Siri ya mafanikio yako imefichwa katika tabia zako za Kila siku", hivyo katika safari yeyote juu ya mafanikio inapaswa kuwa na tabia Zifuatazo kusudi uweze kufanikiwa;

Fahamu unachokitafuta maishani mwako.
Watu wengi maishani mwao hawajui wanatafuta nini, na hii ndio sababu kubwa ya kufeli katika safari ya mafanikio Yao. Ukweli ni kwamba watu wengi wapo bize sana na majukumu Yao ya Kila siku ila hawajui wanachokitafuta maishani mwao. Mwaka 1960 profesa Locke aliweza kufanya utafiti kuhusiana na uwezo wa mtu kuweka malengo na kufanikiwa, utafiti ulidhihirisha kuwa watu ambao wanajua wanachokitafuta maishani mwao Wana asilimia 90 ya kufanikiwa. Uwezo wa kufahamu unachokitafuta maishani mwako ni pale unapoweka malengo kama Miaka 10 baadae utakuwa wapi, utakuwa unafanya nini, utakuwa na pesa kiasi gani, jamii itakuwa inakuzungumziaje? Kuwa na malengo ya kule unakotaka kwenda kutakufanya kuwa na juhudi katika safari ya mafanikio yako.

Jenga kujiamini.
Hapa muhimu ni kufahamu kuwa kiwango chako Cha kujiamini ndio hujulisha kiwango Cha watu wengine kuamini kama unaweza. Kukosa hali ya kujiamini kumewafanya watu wengi kushindwa kufanya kitu ambacho Kiko mioyoni mwao, usiwe mmoja wao hivyo jenga kujiamini na kujithamini katika Kila jambo unalofanya katika safari yako ya mafanikio.

Kufanya mambo Kwa ubora.
Katika maisha ukikutana na kila aina ya fursa inakubidi kufanya fursa hiyo Kwa ubora na Kwa umakini wa hali ya juu Sababu itakufungulia fursa nyingi katika maisha Yako bila wewe kufahamu. Haijarishi ni wapi na kwa wakati gani inakubidi ufanye mambo Kwa ubora, haijarishi unapata faida kidogo namna gani au mshahara mdogo kiasi gani kwani Kila atayehitaji huduma au bidhaa kama Yako ataambiwa aje kwako Kwa sababu unafanya vitu Kwa ubora wa hali ya juu.

Wajibika na maisha yako.
Katika safari yeyote ya mafanikio ni muhimu kujua kwamba maisha Yako ni wajibu wako mwenyewe. Watu wengi walioweza kufanikiwa wanafahamu ni jinsi gani wanawajibika na maisha Yao na sio mtu mwingine. Katika safari ya mafanikio inakupasa uwe na wajibu wa maisha Yako, achana na mawazo ya kutaka kuonewa huruma, achana na visingizio kama vile wazazi ndiyo sababu ya wewe kuwa hapo ulipo lakini jenga bidii na juhudi za kuweza kuwajibika na maisha Yako Kwa asilimia zote kwani unatakiwa kuelewa kuwa unayo nguvu na uwezo mikononi mwako wa kubadilisha maisha yako kuanzia leo ukiamua kutotumia visingizio. Ulivyo leo ni kutokana na maamuzi yako ya jana.

Kuwa na nidhamu.
Katika kuelekea kilele cha mafanikio inabidi uwe na nidhamu. Watu waliofanikiwa huwa wana nidhamu hasa katika maeneo makubwa mawili ambayo ni nidhamu ya muda na nidhamu ya pesa. Nidhamu ya muda ni jinsi ambavyo unatumia muda wako. Hii itaonesha kama utaeza kufanikiwa au usifanikiwe. Hapa inakubidi uweke vipaumbele katika mambo ya muhimu na uache kutumia muda mwingi Kwa vitu visivyokuwa na msingi kama vile kuangalia kurasa za udaku Kwa masaa mawili na kuendelea. Eneo la pili ni nidhamu ya pesa. Hapa inakubidi uwe na bajeti yako mwenyewe na kuhakikisha kuwa unatumia pesa Kwa ufasaha na kuweka akiba itayokusaidia Kwa vitu vingine mbeleni. Ni kuhakikisha matumizi ya mahitaji yako hayazidi pesa uliyonayo kusudi uwe na akiba na kuepukana na matumizi yasiyokuwa na mpangilio maalumu.

Usikubali kukata tamaa.
Katika kuelekea mafanikio Kuna hali ya kutoona mbele au mwanga na hii ni kawaida usiogope. Unachotakiwa kufanya ni kuinuka tena na kutokubali kukata tamaa haijarishi una umri gani na umepitia mangapi. Hebu jifunze Kwa Colonel Harland, akiwa na Miaka 60 alijaribu kujiua baada ya kuona giza mbele yake lakini alisimama tena na kuamua kukopa pesa na kuanza kuuza kuku Kwa kutembea nyumba Kwa nyumba mpaka Leo hii kampuni yake ya KFC inazidi kutanuka, inakuaje kama angeweza kukata tamaa?. Mafanikio yeyote Yale yanaitaji uvumilivu wa hali ya juu sana, haijarishi wangapi watakuacha katika safari yako ya mafanikio usisahau kwamba wewe unapaswa kuwajibika na maisha yako Kwa asilimia zote , usikubali kukata tamaa haijarishi uliwai kufeli huko nyuma.

Kuwa na fokasi.
Mwanzilishi wa kampuni ya vifaa vya elektrioniki ya Apple, Steve Jobs katika mahojiano aliulizwa maana ya fokasi alisema ni uwezo wa kusema hapana Kwa vitu visivyochangia katika malengo yako ya wakati huu. Ni vizuri kutambua kuwa Kuna aina ya watu ambao ukiruhusu kuambatana nao basi utajikuta Kila wakati umetoka nje ya mwelekeo wako. Jifunze kusema hapana Kwa mambo yasiyokuwa na mchango katika safari yako ya mafanikio.

Kufanya maamuzi bila uwoga.
Maamuzi maana yake ni kuchagua mwelekeo wa maisha Yako. Siku zote kumbuka hivyo ulivyo leo ni kutokana na maamuzi uliyofanya jana na vile utakavyokuwa kesho ni kutokana na maamuzi unayofanya Leo. Watu wengi wanashindwa kufanikiwa malengo yao Kwa sababu wamekuwa ni wazito na woga kufanya maamuzi maishani mwao. Unapokuwa mtu ambaye hufanyi maamuzi utakuwa mtu wa msongo wa mawazo juu ya maisha Yako na unajikuta unapoteza fursa muhimu maishani mwako, usiwe mmoja wao maana Kuna vitu yavitabadilika bila kuwa na maamuzi. Utajikuta unapoteza fursa nyingi kutokana na uwoga wa kutofanya maamuzi sahihi, kubali na kuwa tayari kulipia gharama za maamuzi.

Katika kuelekea safari maridadi juu ya mafanikio, inakubidi uweze kujenga tabia hizi za ushindi katika maisha yako kwani utafanikiwa Kwa viwango vya juu. Jitihada za kujenga tabia hizi katika maisha yako itakupa uwezekano mkubwa wa kufanikiwa katika mafanikio yako. Simama imara ukaanze kuishi maisha ya ndoto zako, malengo uliyojiwekea na usiwe mwoga kuelekea katika safari hiyo maridadi juu ya mafanikio,amini unaweza kuinuka tena.
 
Upvote 5

Imekaa vizuri hii
 
TUKUMBUKANE NA WENGINEO

[emoji845]NISAIDIE KUPATA MCHONGO[emoji845]
Nina degree ya
COMMUNITY ECONOMIC DEVELOPMENT.
[emoji419]Naitafutia uzoefu ili badae niweze kuwa na chochote kwenye CV na kuombea Kazi.
Nisaidie hata Internship tu.
Location :KIGOMA ila kokote kama kuna uhakika mimi nitafika.
[emoji736]Msaada waungwana, mniinue
[emoji736]Taasisi
[emoji736]Social Work
[emoji736]Mashirika(NGOS)
kokote kule aisee
0628849189
 
Back
Top Bottom