Safari ya Che Guevara Tanzania 1965

Safari ya Che Guevara Tanzania 1965

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Utangulizi
Katika waandishi ambao siwezi kupita makala zao ni Salim Msoma. Utampenda akiandika au kuzungumza kwa Kiingereza au Kiswahili achilia mbali mantiki katika maudhui. Kaniletea habari hizi hapo chini nami nimeona ni muhimu niweke hapa kwa faida ya jamii. Salim Msoma kanistaajabisha pakubwa kabisa. Nilikuwa nasikia kuwa kulikuwa na vijana wa Kitanzania walikwenda kupigana bega kwa bega na FRELIMO Mozambique wakati wa kupambana na Wareno. Lakini hii ilikuwa minong'ono tu isiyokuwa na yakini. Leo farasi mwenyewe kazungumza na kakiweka chano uwanjani. Salim Msoma alikuwa mmoja wa hao vijana waliovuka mpaka na kuingia Mozambique wakiwa na askari wa FRELIMO bega kwa bega hatua kwa hatua wakilala wote porini. Ningependa kumaliza utangulizi huu wangu kwa kusema kuwa nilialikwa kuzungumza Northwestern University. Evanston Chicago, chuo alichosoma Eduardo Mondlane. Ukumbi niliozungumza ulikuwa ukumbi uliopewa jina lake na picha yake kubwa imetudikwa pale.

SmAiOvZ2FDPxAT2rns6LZEBQdfd0n4QIYqEPj7jLGL5AFg-39JdNK9GivHNLz3UTdfUS3iICuqlYybb3MHHyqxiewSix=s0-d-e1-ft


Picha hii muhimu ilipigwa baina Feb na April 1965 wakati Che alipowasili Dar kwa maandalizi ya kwenda Congo kuwaunga mkono vikundi vya kina Kabila dhidi ya utawala wa dikteta Mobutu.Tarehe 11 Feb Che alizuru Zbar na Mzee Karume akamkabidhi mgeni huyo kwa Ali Sultan huku akimueleza "Sikiliza Ali! Nakukabidhi mgeni huyu 'comrade' mwenzenu uwe nae wakati wa ziara yake hapa Zbar na umhudumie vizuri".Karume hakuwa akielewa uzuri kuwa Che alikuwa tayari anajuana kwa karibu sana na Ali Sultan tangu 1961 kule Cuba wakati ZNP walipokwenda kufungua ofisi Havana.Akaibuka yule shawishi hayati Musa Maisara ikawa kama yeye ndie anaemjuwa na kukabidhiwa mgeni.Kila picha alopiga Che yeye alijiweka ubavuni mwake eti na yeye 'comrade'!

Usiku wa tarehe 12Feb Che alikutana na makomred waliokuwepo Cuba 1962 katika karamu maalum.Siku hiyo walikuwepo Ali Mahfoudh(inasemekana karamu ilifanywa kwake,Migombani),Moh'd Ali Foum,Ali Abdalla Bafakih,Salim Ahmed n.k.

Bahati mbaya makomred wa jeshini wote walikuwa wamepelekwa Urusi (sijuwi kama Jiwe na Ali Mshangama walikuwa tayari wameshapelekwa Indonesia).Kwani Che aliwaulizia na alisikitika sana kuwakosa kuonana nao.Che alipewa nyumba ya kukaa na Ali Sultan pale Beit-Ras nyumba ambayo aliwahi kukaa Mr Amour Ali Amer na hadi leo imewekewa kibao cha kumbukumbu (plaque) ya ukaazi wake kwenye nyumba ile.

Ziara ya Che Zbar ndio hasa iliyofichuwa habari kuwa Mwanamapinduzi huyo alikuwa Tanzania kwani kabla hapo hakuonekana popote rasmi.Ilifika hadi Balozi wa Marekani Dar kulalamika kwa Nyerere kuwa walikuwa na Intelligence kuwa Babu alikuwa pamoja na Commandante huyo.Mwalimu bila shaka alijua kuwa Che yuko in town lakini alijifanya hajui na eti kumuuliza Babu endapo kweli yuko nae mtu huyo! Janab nae aliruka na kusema kuwa hakumtia machoni mwake.Inasemekana Che aliondoka Dar kwenda msituni Congo mnamo wiki ya mwisho ya mwezi Apri 1965 na alikaa huko hadi Oktoba 1965 yaani miezi kama sita.Aliporudi Dar alijifungia ndani ya jengo la

Ubalozi wa Cuba hadi Feb 1966 akiandika Diary na kumbukumbu zake huko Congo.Ni mtu mmoja tu ndie alikuwa akijuwa uwepo wa Che Dar kipindi hicho chote.Nae ni Al-marhum Janab ambae alikuwa ni muekaji siri mzuri katika mambo haya ya struggle.Nakumbuka hata mimi mwenyewe nipokuwa najiandaa ku-infiltrate across mto Ruvuma kwenda msituni Mozambique na vikosi vya Frelimo (1968) mtu pekee ambae alikuwa akijua hatari hiyo alikuwa Babu kwasababu tulikatazwa kueleza kwa yeyote na viongozi wa Frelimo. Hata Serikali ya Tanzania ilikuwa haijuwi.Mimi nilimdokezea just in case endapo nitapotea akamno'goneze baba yangu.Naam alificha siri mpaka tumerudi baada ya miezi 3 porini.Na hapa lazima niseme sisi katika ujana ule tulikuwa 'inspired' na Che Guevara.

Salim Msoma
 
Iko poa Sana ebu endelea huwa unanifurahisha Sana ila mambo madogo sometimes napinga.you are bravo
 
Mleta uzi very thanks,hii ni habari njema kupata kuisikia coz ya kale dhahabu ukizingatia inamuhusu CHE
 
Naam ngoja tuandae jamvi. Hii habari haifai kuikosa. Maalim Mohamed Said lete uhondo!
 
Naam niandae jamvi. Hii habari haifai kuikosa. Maalim Mohamed Said lete uhondo!
Kwezisho hiyo kaniletea Salim Msoma nami nikaona niilete barzani. Kilichonivutia ni yeye kwenda kupigana Msumbiji.
 
Kwezisho hiyo kaniletea Salim Msoma nami nikaona niilete barzani. Kilichonivutia ni yeye kwenda kupigana Msumbiji.
Mzee ms inaonekana viongozi wengi wa znz ya nyuma ya miaka 1970 walikuwa na uhusiano wa hali ya juu na serikali ya cuba?
Nakama ndio hivyo nini kimeondoa urafiki huo mkubwa uliokuwepo baina ya nchi hizi mbili znz na cuba?
 
Afadhali hata utuletee mambo mengine ,sio kila siku Zanzibar hiki ama uislamu vile ,
 
Mzee ms inaonekana viongozi wengi wa znz ya nyuma ya miaka 1970 walikuwa na uhusiano wa hali ya juu na serikali ya cuba?
Nakama ndio hivyo nini kimeondoa urafiki huo mkubwa uliokuwepo baina ya nchi hizi mbili znz na cuba?
Sahimtz,
Si rahisi kulijibu swali lako kwa sentensi mbili tatu kiasi cha mtu
kuelewa ilikuwaje Zanzibar ikakumbwa na siasa za mrengo wa
kushoto.

Jana Salim Msoma mmoja wa vijana waliokuwa na hamasa hizi
kaniandikia kunieleza kwa muhtasari hali ya siasa ya wakati ule.

Ingia hapa:
Mohamed Said: SALIM MSOMA AELEZA KICHWA CHA HABARI: BADAWI QULATEIN ALIANZA KAMA ''COMRADE'' AKAMALIZA KAMA SUFI
Mohamed Said: SALIM MSOMA ANAELEZA SAFARI YA CHE GUEVARA TANZANIA 1965

Kitu kilichokuja kufifilisha uhusiano huu ni muungano wa Zanzibar
na Tanganyika mwaka wa 1964.

Baada ya mapinduzi ilionekana waliokuwa na uoni wa kuendesha
serikali walikuwa ''vijana wa Abdulrahman Babu'' na Babu yeye
alikuwa na uhusiano mkubwa sana na China na Cuba.

Karume alikuwa na hofu ya wasomi na kwa ajili hii aliona salama
yake itapatikana chini ya mbawa za Nyerere.

Nyerere aliitaka Zanzibar kwa sababu ambazo hazikuoana na azma
waliyokuwanayo wafuasi wa Umma Party (UP) ingawa kwa wakati
ule UP ilikuwa ishafutwa na wanachama wake kujiunga na ASP.

Ule uoga wa Karume wa wasomi ukampelekea yeye kuwahamisha
wanamapinduzi wengi vijana wa mrengo wa kushoto kama Babu,
Hanga na Salim Rashid na wengineo kuja Bara.

Hii ilikata ule uhusiano uliokuwapo kati ya vijana hawa na Cuba kwa
kuwa hawakuwa tena na uwanja wa kufanya siasa mbele ya uso wa
Nyerere.

Ingia hapo chini kupata jibu la swali lako kwa kirefu ingawa katika
suala la mapinduzi na ushiriki wa makomredi hii inahitaji maelezo
kwani makomredi hawakushiriki katika mapinduzi kama inavyoeleza:
Abdulrahman Babu: Tanuru La Mapinduzi Zanzibar Na Muungano Lisilokumbukwa VIII – Raia Mwema
Mohamed Said: MASAHIHISHO: SALIM RASHID NA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

20121124_174030.jpg

Mwandishi akifanya mahojiano na Salim Rashid Katibu wa Kwanza wa Baraza la Mapinduzi 1964
TV Imaan Kipindi: Walioacha Alama Katika Historia

Nimekuwekea rejea kadhaa.
Si rahisi kujibu swali kama hili lako inahitaji muda na rejea kadhaa.

Lakini ikiwa unataka kuijua historia hii soma kitabu cha Dr. Harith Ghassany,
Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru na soma kitabu cha Ali Muhsin, ''Conflicts and
Harmony in Zanzibar.''

Kuna mengi yatakayo kustaajabisha kabisa.
 
Back
Top Bottom