Safari ya matumaini ya Tanzania kuelekea Fainali za Afrika 2019

Cardinal06

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2015
Posts
963
Reaction score
326
Habari wana familia ya mpira wenzangu.

Tumeongea mengi na tumesoma mengi kuhusu kukua kwa mpira wetu Tanzania. Binafsi naona wanachi wengi tunakosoa kuliko kutoa ushauri wa nini kifanyike.

Nimekaa nimeona nije na ushauri huu ambao naamini pale nilipoishia kuna Mtanzania mwenzangu atakua na jicho la ziada ataongezea au atapunguza pale nilipozidisha au kupunguza lengo likiwa ni kujenga kuliko kulaumu tu.

{1}. Ili kuanza kutengeneza msingi imara wa mpira wetu,tuamue kwamba kila timu ya ligi kuu nilazima iwe na timu C ya under 17 na tuweke ligi kuu ya vijana hawa wa under 17, kama huna timu hii basi unapoteza uhalali wa kucheza ligi kuu.

{2} kila timu ya ligi kuu ni lazima iwe na timu B yaani under 20 na tuweke ligi kuu ya vijana wa umri huo na tutafute bingwa wake kwa msimu mzima na kama huna timu hii unapoteza uhalali wa kushiriki ligi kuu.

{3} Mashindano haya ya vijana yasifanyike kama bonanza kuwaita sehemu moja, bali iwe ligi kama ilivyo ligi kuu. kila timu icheze nyumbani na ugenini na hapa kama timu yako A inayoshiriki ligi kuu itashuka daraja basi na timu zako zote unashuka nazo kwenda kujiunga na daraja la kwanza bila kujali timu yako B au C ilishika nafasi ya ngapi kwenye ligi TWO au ligi TREE ili kutoa nafasi kwa zile timu zitakazopanda zipate nafasi kwenye timu a,b na c .

{4} Na kwa timu za daraja la kwanza pia kanuni itakua hiyo lazima uwe na timu hizo ndio upate uhalali wa kucheza ligi daraja la kwanza. Mimi naamini tukisimamia vizuri na kuwa wakari na lengo moja hapa tutakua tunatengeneza msingi imara wa soka letu na kuepuka lawama hizi tunazotupa kwa viongozi wetu wa TFF na kocha bila kuangalia tumekwama wapi. Timu hizi za vijana sio ziwe kwenye makaratasi tu bali zionekane kweli zipo na jicho letu tulitupie sana huku.

Naamini haya yakifanyika tutatumia ligi hizi kuvuna vipaji nchi nzima kwa ajili ya timu zetu za Taifa kuanzia ile ya under 17, 19,20 na
senior team.

Nchi nyingi zimeendelea duniani kwa kuacha uvivu na kuwekeza kwenye soka la namna hii na mwisho wamefanikiwa.

Chanzo: MpenjaBlog

 
ni wazo zuri....lakini napata swali ambalo tunaweza kubadilishana mawazo...hivi timu kama NDANDA inapata pesa kwa kutembeza bakuli mitaani, itaweza kweli kuhudumia SAFARI na KAMBI za timu A,B na C??.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…