Safari ya miaka 9 tangu kuacha kazi. Hamasa kwa vijana wenye maono makubwa

Huu uzi hata kama mtu anataka kuacha kazi lazima aogope akiusoma. Imagine msoto wa miaka yote hyo🤣🤣. Kwanini usingekopa hata Million 10 ndo uache kazi ukiwa na Mtaji wa kueleweka?
Si utadaiwa na benki au
 
Biashara gani hiyo?
 
Lakini umepoteza muda sana, yaani miaka yote 9 umeitumia kupata elfu kumi kwa siku sawa na mwanafunzi wa chuo kikuu anayepokea boom?
 
Kutumia watu bila maokoto🙄 atafika huko acha atumie alichonacho kwanza.
 
Mimi mishe zangu kwa siku inabidi ziniletee laki moja+, lakini kuna siku unakuta nimeamka nimechoka alafu sina ile energy ya kuingia pori kuzitafuta hela hivyo nabakia kuzuga kitaa na ujuzi wangu lakini sikosi 50k mpka 60k.....
 
Common myths in entrepreneurship,
- It's an easy way to get rich
-The idea is everything
-Entrepreneurs are born to lead
-It's all on your shoulders
-You know the secret to success

Kuna kukatisha tamaa… na kuna kuambiwa uhalisia.
 
Si utadaiwa na benki au
Hapana.... Kuna jamaa namfahamu alikuwa mwalimu, jamaa ni risk taker alichukua mkopo km 8m akapiga chini kazi.. Huo ni mwaka 2020 kaanza biashara sasa hivi ule mshahara wa mwalimu aliokuwa anapokea nadhani anauingiza ndani ya siku kadhaa😁
 
Hongera sana Mkuu,mimi nina almost miezi 8 tangu nimeacha kazi katika ile Halmashauri.
 
Kwa hongera sana,nimejifunza jambo moja hasa kwa sisi wabongo tunashindwa kuendelea kwa kuwa tunasikiliza wapendwa wetu wanasema juu ya maamuzi yetu,kujikana na kuwakana uwapendao ni maamuzi magumu lakini mazuri kwa cku za usoni.
mfano:kuna mwamba aliamua kukata mawasiliano na kila mtu wa kwao akatokomea kenya kwa miaka 5+ alivyorudi ni bonge la tajiri.
 
Yaani 3 mil tu akaacha kazi na karudi tena kule kule kwenye ualimu.

Angesubiri hata akakopa mkwanja mrefu ndo akaacha kazi
Afadhali ya huyo Emma,mimi niliacha kazi bila hata Mia pesa ya nauli niliuza kitanda,godoro na mtungi wa gesi, nikapata pesa ya nauli basi Sumri toka katavi to Mbeya to Iringa pesa iliyobaki nilinunua konyagi za viroba na kula njiani ,nilifika Iringa sina hata Mia,nilivoonana na ndugu zangu wote tukaanza kulia kwa pamoja.Jamani stories yangu ni ajabu ya Emma ikasome,hakuna aliejua nitatoboa tena,wakati naacha kazi nina mke na watoto watatu,nashukuru mke hakuniacha hadi leo nana watoto 6 nae,tuna nyumba nne za biashara za kupangisha na moja ya kuishi,biashara imesimama,watoto wanapiga shule,biashara za safari,nk.Ila katika maisha haya binadamu wanaroho mbaya sana kwani ilifikia wakati nikawa natembea na kamba ya kujinyonga popote nitakapoona site nzuri.But Mungu,Mama yangu,Mke wangu na watoto wangu hawakunitupa.Popote ulipo kiongozi wa taasisi husika uliyenisababishia kuichukia kazi ya kuajiriwa Mungu akulaani na kizazi chako,ulidhani sitafika mbali lkn Mungu alikukwamisha,ila WAIRAQ wana roho mbaya,
 
Aiseee,kweli ulijilipua

Mimi naogopa sana haya maisha,siwez jaribu hyo risk tena nikiwa na familia!
 
Nimesoma Makala Yako kama robo 3 sijamaliza too long.

Moja ya sifa zako ni moyo wa kupambana sana unfortunately hapa Duniani wanaofanikiwa zaidi hawatumii.juhudi na maarifa pekee Bali Nguvu za Giza.

Nimegundua kama ulivyosema kipaji chako kikubwa ni uandishi na hapo ndipo ungeweka Nguvu zaidi.

Pia Nguvu uliyotumia kuanzisha tuition ungeiweka kwenye kuanzisha nursery school nadhani ungekuwa mbali zaidi hususani ungekuwa kwenye Mikoa ambayo Haina ushindani sana tofauti na hapo ulipo Kuna ushindani wa Elimu zaidi.

Mwisho nikupongeze Kwa kujituma ila sio kweli kwamba Ukiwa Muajiriwa huwezi kuwa Tajiri,hizo ni fix za watu tuu na Mimi nitakuwa Tajiri Kwa Muajiriwa maana inategemea na connection gani umeweka na aina ya shughuli unafanya.
 
Mkuu naomba unielezee kidogo kuhusu hapa uliposema nguvu za giza, Nimekuwa nikisikia sana kuhusu utajiri wa nguvu za giza... Huo ukoje??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…