Safari ya miaka 9 tangu kuacha kazi. Hamasa kwa vijana wenye maono makubwa

2012 miaka 28 basi 2024 utakuwa na miaka 40 siyo 36 acha kudanganya
 
Asante kwa hii elimu nimejifunza kitu
 
Kwenye nimesema mwaka huu nina 36.....pia nimesema niliacha kazi mwaka 2015 nikiwa na miaka 27..... Hiyo 2012 unayoisema nimeeleza kuwa ndio mwaka niliomaliza chuo nikiwa na miaka 25....So by 2026 nitakuwa na miaka 38 sio 40 mkuu.

By the way miaka sio ajenda kuu kwenye andiko langu. Lengo kuu la andiko ni kuwapa watu nafasi ya kujifunza kitu kutoka katika mapambano yangu.

Anaweza kujifunza makosa niliyofanya akayarekebisha na kufanya vema zaidi. Pia mwingine anaweza kujifunza ubora wangu na akafanya vema pia.

Samahani sana mkuu kama nitakuwa nimekuudhi.

Kasome wewe vinzuri

Asante kwa hii elimu nimejifunza kitu
Asante sana mkuu. Barikiwa sana
 
Aya bhana
 
Hongera sana. endelea kupambana bila kukata tamaa. penye nia pana njia.
 
Bado sijaona point ya utajiri hapa , miaka 7 bado unafundisha mwenyewe kwenye hiyo tuition centre 😁 hapa nilitegemea uniambie una walimu10 ambao unawalipa, , umefanikisha kuipata biashara ya kukuingizia elfu10 Kwa siku na unatupa miaka2 tutakuona level za akina Mo?? Seriously 😃 , huna nyumba, huna kiwanja , huna hata usafiri , then unakuja kuanzisha Uzi wa mafanikio😃😃

Nilichogundua kimoja hukujipanga wakati unacha Kazi urikurupuka Bila kujua nini exactly unaenda kufanya baada ya kuacha Kazi , Milion 3 sio ya kutukana mamba😂😂😂
 
Mkuu sijasema kuwa nimefanikiwa. Kwenye uzi nimesema watu wajifunze kupitia mimi. Ila nimesema katika kupata hiyo elfu 10 per day na kupitia uzoefu niliopitia miaka 9 nina uhakika wa kuwa Mo. Hiyo ni up to wewe uamini au usiamini but nakuhakikishia nitakuwa Mo. Mpya hapa mjini miaka sio mingi.


Ndugu katika kuhaso kuna kujifunza vingi, kuna kujua mengi, kina kukomaa na kuna kujifia zaidi. Ogopa mtu anayejifunza kutokana na failure kwa muda mrefu. Siku gari lake likiwaka ni moja kwa moja mpaka mwisho wa safari.

Asante kwa kusoma uzi wangu na kutoa mchango wako ambao japo unaonekana ni wa kukatisha tamaa but kwangu hiyo ni mojawapo ya sababu za kwa nini lazima mimi nije kufanikiwa.

Mwisho nikukumbushe kitu kimoja katika vingi nilivyojifunza. Utajiri/mafanikio sio kuwa na nyumba, kuwa na kiwanja, kuwa na pesa, kuwa na nguo nyingi. Bali utajiri ni matokeo ya akili smart inayowaza na kutenda mqmbo kinyume na mazoea. Ni akili inayokwenda kinyume na mtazamo wa wengi ili kufanya imposible kuwa possible. Mtu akifika hatua ya kuwa na akili ya namna hiyo huyo tayari ni tajiri mtarajiwa. Asante.
 
Awali ya yote nasema nimejitahidi kusoma uzi wote na kunameng sana.

Nikupe pole kwa yote magumu na changamoto ulizopitia.

Pongezi kwa uthubutu uloufanya.

Mengi ya kujifunza yako hapa
 
Mkuu kitu kimoja uelewe ukiwa na maono makubwa ni ngumu sana watu wa kawaida au wenye mawazo madogo kukuelewa...wao wanaona boundaries tu like umri umeenda,, Hela hyo elfu kumi ndogo kwa siku,, sijui hujawah miliki mil 50, mara mawazo hayo hayawezekan.....nk

But ww keep focused na ulichopanga..watu wa hvo wapo kila sehem hata mm walinisumbua sana kipind naanza biashara na kuachana na mamb ya kuajiriwa..

All in all usisahau ibada kwa iman Yako ..amka usiku saa nane pakiwa tulivu jiconect na holy power daily,,mamb yatafunguka kwa uraisi zaid..

I pray for you comred!!
 
Shukrani sana mkuu. Ubarikiwe sana kwa kunitia moyo.
Awali ya yote nasema nimejitahidi kusoma uzi wote na kunameng sana.

Nikupe pole kwa yote magumu na changamoto ulizopitia.

Pongezi kwa uthubutu uloufanya.

Mengi ya kujifunza yako hapa

Asante sana mkuu kwa kuelewa kusudi la bandiko langu na kunitia moyo. Ushauri wako wa maombi usiku nitafanyia kazi vema. Asante sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…