African Believer
JF-Expert Member
- Jul 30, 2015
- 436
- 426
Pierre Konk Liquid, ni jina maarufu sana kwa sasa si tu kwenye mitandao ya kijamii bali hata mitaani kote katika eneo la Afrika Mashariki kwa ujumla.
Pierre, mtu ambaye kwa sasa ameanza kupata pesa kupitia maisha yake halisi ya kilevi baada ya vipande vya video kumuonesha akiwa amelewa chakari na kupelekea kupata umaarufu mkubwa. Kitu kinachowashangaza watu wengi, lakini lakini mshangao huo si katika ulimwengu wa nyota (fate)
Umaarufu wa Pierre umekuja tu pasipo yeye kupanga wala kutarajia. Alikuwa na amekuwa ni mlevi ambaye akishamaliza shughuli zake za kila siku hukimbilia baa kupata kilaji, na anasema hiyo ndiyo starehe yake anayoipenda.
Maisha na umaarufu wake unahusiana vipi na nyota (fate)?
Kwa sisi tunaoamini katika nyota (fate) tunaamini kuwa kila jambo linalimtokea mwanadamu limeshapangwa miaka mingi iliyopita na kilichosubiriwa ni wakati tu wakutokea na wala haihitajiki jitihada ya namna yoyote ile.
Katika ulimwengu ulioratibiwa tokea awali, kile aliye katika nafasi fulani amekuwa hapo kwani ilishapangwa na mwisho wake pia ulishapangwa.
Katika ulimwengu huu kufanikiwa au kutokufanikiwa hakutokani na kiwango chako cha kufanya kazi wala namna ulivyo mvivu. Mafanikio huja tu sawasawa na kuanguka.
Mwisho kabisa, niseme tu lipo funzo la kinyota kwenye umaarufu wa PIERRE.