Safari ya Sam Nujoma

Safari ya Sam Nujoma

Joined
Oct 5, 2015
Posts
90
Reaction score
482
Harakati za Sam Nujoma!

Kwa ufupi...
...Mamia ya wakimbizi kutoka kusini-magharibi mwa Afrika walifanikiwa kutoroka kwa msaada kutoka vikundi vya wapigania uhuru wa mataifa mengine lakini zaidi kwa msaada wa serikali ya Tanganyika.

Kulikuwa na njia kuu mbili za kutoroka kutoka kusini-magharibi kwenda Tanganyika; moja ilipitia Rhodesia ya kusini kisha Rhodesia ya kaskazini na hatimaye Tanganyika. Njia ya pili ilipitia Angola kisha Rhodesia ya kaskazini na hatimaye Tanganyika.

Sam Nujoma alikuwa moja ya wakimbizi wa mwanzo waliotoka kusini-magharibi kuelekea Tanganyika. Nujoma aliamua kutoroka kutoka Kusini magharibi mwa Afrika hadi Tanganyika kutafuta hifadhi baada ya kushitakiwa kwa kesi ya kusababisha vurugu. Ili kuepuka jela alianza safari yake mnamo februari mwaka 1960 akiwa na kusudio la kusoma nje ya Afrika, nafasi ambayo angeipata kutokea Tanganyika.

Safari ya kutoka kusini magharibi mwa Afrika (Namibia ya leo) ilimgharimu muda wa miezi miwili, akitumia namna tofauti tofauti za usafiri hasa kutembe kwa miguu. Alitembea, alipanda treni, magari na mara chache ndege akipitia Bechuanaland (Botswana ya leo) Rhodesia ya kusini (Zimbabwe ya leo), Rhodesia ya kaskazini (Zambia ya leo), kisha Congo na hatimaye Tanganyika.

Akiwa ndani ya treni kutoka Bechuanaland kuelekea Rhodesia ya kusini, Sam Nujoma alijifanya raia wa Nyasaland aliyehamia Bechuanaland na sasa yupo safarini kurejea kwao. Alifanya hivyo kuepuka kukamatwa na maofisa wa uhamiaji wa Rhodesia.

Msaada wa watu wa chama cha National Democratic Party (NDP) huko Rhodesia ya kusini na watu wa chama cha United National Independence Party (UNIP) wa Rhodesia ya kaskazini ulisaidia kumfikisha Sam Nujoma mjini Mbeya alipopokelewa na wanachama wa TANU.

Watu wa TANU walimficha Nujoma huko mjini Mbeya ili asikamatwe na serikali ya kiingereza. Akiwa mjini Mbeya, Nujoma aliugua Malaria na kukimbizwa hospitalini ambapo alilazwa kwa ajili ya matibabu.

Lakini kabla ya kuruhusiwa alitoroshwa na watu wa TANU baada ya kugundua kuwa serikali ya kikoloni (waingereza) wanamtafuta, kisha walimsafirisha kwa siri hadi mjini Dar Es Salaam alipokutana na

Nyerere mnamo Aprili 1960. Akiwa mjini Dar es Salaam Nujoma alipatiwa hati ya kusafiria ya Tanganyika kwa msaadsa wa rais wa TANU, Julius Nyerere. Baadaye alipata nafasi ya kuzungumza na kamati maalum ya umoja wa mataifa huko mjini New York.

Kutokea Tanganyika, Nujoma alisafiri hadi Khartoum, Sudan kisha Acra, Ghana alipohudhuria mkutano ulioitishwa na Kwameh Nkuruma, ukilenga kupinga kitendo cha nchi ya Ufaransa kufanya jaribio la bomu la atomiki katika jwanga la Sahara.

Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Patrice Lumumba, Joseph kasavubu, Gamal Abdel Nasser na Frantz Fanon. Baada ya mkutano, Sam Nujoma alisaidiwa na Kwame Nkuruma kusafiri hadi mjini New York nchini marekani kuzungumza na kamati ya umoja wa mataifa iliyoshughurika na masuala ya kusini magharibi mwa Afrika.

Moja kati ya mambo aliyotaja katika hotuba yake kwa kamati hiyo ni uhuru wa Afrika ya kusini magharibi, akisisitiza upatikane si baada ya mwaka 1963.
\
Mwaka 1961 alirudi mjin Dar es Salaam, ambapo alianzisha rasmi ofisi ya makao makuu ya chama cha SWAPO, akisaidiana na wanaharakati wachache wa ‘Afrika’. Kisha alianzisha mchakato wa kutoa ufadhili wa masomo kwa watu kutoka Namibia, pamoja na mafunzo ya kijeshi ya kuikomboa Namibia.

Baadhi ya wanaharakati walikuja kumuunga mkono ni Mzee Kaukungwa, Mose Tjitendero na Hifikipunye Pohambwa aliyekuja kumrithi Nujoma katika kiti cha Urais wa Namibia mnamo Machi 21, 2005 hadi Machi 21, 2015.

Kwa Baraka za Julius Nyerere, Sam Nujoma na viongozi wengine wa harakati za ukombozi wa Afrika, walifanya walichotaka ndani ya Tanganyika, wakijiandaa kuzikomboa nchi zao kwa mtutu wa bunduki.

Ndani ya chama cha SWAPO, Nujoma alianzisha kikundi cha kijeshi kilichoitwa SWALA (South West African Liberation Army (SWALA) ambacho baadae kiliitwa PLAN (People’s Liberation Army of Namibia).

Kikundi hiko kilikita kambi huko mjini Kongwa Dodoma, kambi kubwa kuliko makambi yote ya Afrika yaliyohodhi wapiganaji wa ukombozi wa Africa. Kongwa ilikuwa pia kambi ya kwanza kujengwa barani Afrika kwa ajili ya kuwapatia mafunzo wapiganaji kutoka makundi ya kijeshi ya vyama vya ukombozi vya kusini mwa Afrika.

Nujoma alifanikiwa kupata silaha kutoka Algeria, kupitia Misri, pia Sudan, Tanzania na Zambia, na kisha zilisafirishwa hadi kijiji cha Omugulugwombashe katika mji wa Ovamboland, kaskazini mwa Namibia.

Wakati huo Namibia ilikuwa chini ya utawala wa makaburu wa Afrika kusini. Nujoma na wenzake walikuwa na kesi katika umoja wa mataifa kutokana na makosa ya kusababisha vurugu zilizopelekea mauaji. Kesi hiyo pamoja na maonevu mengine yaliwafanya akina Nujoma kuhamisha shughuli zao za kisiasa na kuishi uhamishoni, Tanganyika.

Katika kesi iliyokuwa ikisimamiwa ana mahakama ya umoja wa mataifa, The Hegue, makaburu wa Afrika kusini walidai kuwa Nujoma na wenzake walijikimbiza wenyewe, na kwahiyo kuishi kwao uhamishoni ni maamuzi yao binafsi, na si kwa sababu ya maonevu ya serikali ya makaburu.

Kutokana na utetezi huo, mnamo Machi 21, 1966 Sam Nujoma na Hifikipunye Pohamba walipanda ndege kuelekea mjini Windhoek, Namibia ili kupima imani ya serikali ya makaburu. Lakini walipotua tu, walitiwa nguvuni na siku iliyofuata walihamishwa nchini Zambia.

Miezi mitano baadae, Augosti 26, 1966 askari wa serikali ya makaburu walivamia kikundi cha SWALA katika kambi la Omugulugwombashe. Uvamizi huo ndio ulikuwa mwanzo wa vita iliyoitwa VITA VYA UHURU WA NAMIBIA, vilivyodumu kwa miaka 25...

#Simulizi_za_wazalendo
 
Attachments

  • unnamed (4).jpg
    unnamed (4).jpg
    33.6 KB · Views: 69
  • images (20).jpeg
    images (20).jpeg
    12.2 KB · Views: 70
Safi sana Mkuu kwa historia hii muhimu, Tanzania ilikuwa Mekka ya ukombozi barani Afrika, mahali patakatifu linapokuja suala la ukombozi wa mtu mweusi. Sio tu katika kuandaa wapiganaji kijeshi lakini pia Tanzania ilikuwa ndio makao makuu ya fikra halisia za kujitegemea na kujikomboa kimawazo kwa Mwafrika na mtu mweusi popote alipo. Ni mpaka sasa au tumebadirika….????!!!
 
Kumbe hii barabara ya Sam Nujoma ni jina la Mtu wa Namibia?? Asante Cirillo kwa historia iliyotulia.
 
Safi sana Mkuu kwa historia hii muhimu, Tanzania ilikuwa Mekka ya ukombozi barani Afrika, mahali patakatifu linapokuja suala la ukombozi wa mtu mweusi. Sio tu katika kuandaa wapiganaji kijeshi lakini pia Tanzania ilikuwa ndio makao makuu ya fikra halisia za kujitegemea na kujikomboa kimawazo kwa Mwafrika na mtu mweusi popote alipo. Ni mpaka sasa au tumebadirika….????!!!
Tukisema hata sasa tuna fikra adhimu kama za watangulizi wetu, nadhani tutaibua mdahalo mkubwa sana.
 
Back
Top Bottom