Sibonike
JF-Expert Member
- Dec 23, 2010
- 17,296
- 18,027
Kama unafuatilia seriously maslahi ya kushiriki michuano ya vilabu vya Afrika, utakubaliana nami kwamba vilabu vinaanza kupata mamilioni ya ruzuku kutoka CAF iwapo vitafikia walau ngazi ya robo fainali, na fedha zinaongezeka kadiri unavyokuwa juu. Kuna fungu la timu iliyofika robo fainali, kuna fungu la timu za nusu fainali, mshindi wa tatu, wa pili na bingwa. Lakini watu kwa kuwa hawaijui biashara hii wanadhani aliyeshiriki akaishia 16 bora anaweza kumtambia asiyeshiriki! Kama unashiriki kwa sifa it's okay, lakini kama unashiriki kwa ajili ya biashara, ni heri usishiriki kuliko kupata hasara kwa kushiriki ukatolewa 16 bora
Kwa hiyo Simba licha ya kushiriki mara chache kuliko Yanga, imefaidi hela za CAF zaidi. Ilishafika hatua zote za juu, yaani robo fainali, nusu fainali na fainali, na pia kushika nafasi ya tatu katika makundi
Haina ubishi kwamba Simba ilifikia hatua za juu kwenye ushiriki wake CAF. Je kuna nini cha kuonyesha kutokana na kufaidika huko na hizo hela za CAF? Labda ungesema mwaka fulani Simba ilipata kiasi fulani ikajenga uwanja wake. Umaskini wa timu zetu ni ule ule. Bado tunategemea hela za watu binafsi. Ndio maana UEFA wameanzisha financial fair play. Time lazima iishi kwa mapato na matumizi yake!