Safari za Kikwete nje zimegharimu kiasi gani?



Umekumbusha na kesi ya Liyumba.. ukifuatilia mahojiano ya mwanzo ni kwamba Liyumaba ameshashainda kabla kesi haijaisha .. kwa hiyo ni vizuri wananchi wakaandaliwa kisaikolojia wasije kupiga kelele kama kwa Zombe.. ..
 
This guy has got mipira aisee....mipira in kiinglishi....kudos Lus
 
Kwasababu ni vema pia kulijua hilo, Tusilichukulie hili kama jambo la mzaha mzaha, Nilazima tuliona kama tuna haki nalo, Ni kwafaida na hasara kiasi gani safari za Rais wetu zimetuletea hapa nchini.

Kwa wale wenzetu waishio USA, na nchi za Ulaya wanaweza kutupa tathimini angalau ya safari moja kutoka Tanzania kwa first class hadi USA inagharimu shilingi ngapi kisha tuzidishe na wale wanao ongozana na Rais wetu ,Baada ya hapo tupate gharama za hotel wanazo fikia na kwamuda ule watakaa kaa pale na fedha za chakula na Posho zao.

Am sure the gharama inaweza kujenga Zahanati yenye maabara ya kisasa kabisa au clinic za mama wajawazito za kisasa kabisa kule vijijini..!

Kuna faida gani kwa kugharimia safari za Rais ambazo niza kwenda kutafuta wawekezaji ambao hata kodi hawalipi na wakilipa ndio hizo zipitazo kwenye mikono ya wajanja wachache, mikataba yenye mingine mwaenda kuisainia Ulaya wakati ofisi zenu zipo Tanzania.

Tumekuwa wajinga kwa muda mrefu lakini itafika mahala pakusema inatosha sasa..!
 
Mbona Mugambe hasafiri sana, Mbona Nelson Mandela hakuwa anasafiri sana ? kwanini iwe sisi sisi Watanzania ? Au kwa vile tunajua kusafiri na kwenda kuomba sana ?

Nakumbuka kuna mheshimiwa mmoja alikuwa anapigizana kelele na watu wanaoishi Ulaya kwamba Tanzania ni nzuri na watu wanaishi vizuri kuliko wale waishio huko Ulaya.

Kwanini tunajidanganya ? Kwanini hatuwezi kusimama na kusema ukweli ?

Tanzania watu tunaishi vizuri mijini tu, Tembelea vijijini , Utalia , Hakuna huduma za afya hakuna vyakula vyakutosha ,maji safi hakuna, watu wanaishi kwenye nyumba za udogo tena zile za karne ile ambayo hata mimi siifahamu ,Hili ni Tatizo,Kama hatutoweza kuliona hili kama ni tatizo basi Watanzania hatutoweza kubadirika...Kwa karne tuliyo nayo sasa si Jambo la kufurahia hata kidogo,tumeachwa mbali sana na dunia hii..
 
Swala sidhani kama safari zime gharimu shilingi ngapi. Hilo pia ni muhimu lakini swala la kujiuliza ni safari hizo za nje zimeingizia taifa shilingi ngapi? Je hizo safari zilikua na faida au zilikua upotezaji tu wa vijisenti tulivyo navyo? Cost is not as important as opposed to measuring the gain or loss.
 

Solomon son of David .....

500,000 us dollars?! ni vitu kiasi gani unaweza kununua au kufanya Tanzania kwa hizi pesa?
 
Usiangalie tu kuwa katumia kiasi gani, vile vile angalia kuwa zimeingiza kiasi gani. Nafikiri hicho ndicho cha muhimu sana.

Kwasababu mfanya biashara siku yake huwa si asubuhi, bali jioni wakati anapohesabu faida. Tuishi kiuchumi!

Labda wewe useme ni kiasi gani zimeingiza kama hiyo namba unayo. Na je, una hakika kuwa hizo pesa (kama zipo) zisingetolewa na wafadhili kama VDG asingekwenda huko kufanya umatonya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…