mamayeyo
Senior Member
- Apr 4, 2012
- 167
- 138
Nawapongeza walimu wa Mbeya kwani wameonyesha mshikamano na ujasiri wa hali ya juu kwa kwenda kumkabili mwajiri wao kudai haki zao. (chanzo: ITV taarifa ya habari leo saa mbili usiku). Jinsi walimu walivyo watiifu wameamua kwenda kwa bosi wao wakati wa likizo ili wasipatikane na hatia ya kuambiwa wamegoma kufundisha. Serikali kuu inatakiwa imwajibishe mkurugenzi huyu kama kosa ni lake ili wakurugenzi wengine wapate fundisho wajirekebishe. Bravo walimu wa Mbeya!!!!!!! Kitendo hiki ni meseji kwa wakurugenzi wote wa wilaya kuwa iko siku wanyonge wanaowanyonga watakuja kuwadai haki zao kwa sauti moja.