Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Kinyesi cha binadamu hubeba aina nyingi za vimelea vya magonjwa. Baadhi ya vimelea hivyo ni Salmonella ambavyo husababisha homa ya matumbo (typhoid) pamoja na Norovirus ambao husababisha kuharisha na kutapika.
Pia, choo hubeba E. coli 0157, aina ya bakteria wanaosababisha maumivu makali ya tumbo, kuharisha damu pamoja na kutapika. Kwa watoto, bakteria hawa wanaweza kusababisha homa kali, kufeli kwa figo, kuweweseka pamoja na degedege.
Ni rahisi sana kwa vimelea hivi kuingia ndani ya mwili wa binadamu kwa kuwa mikono hutumika katika kujisafisha baada ya kutimiza hitaji la mwili la kutoa haja kubwa. Aidha, mikono inaweza kugusa sehemu yoyote ya choo ambayo ni rahisi kwa vimelea hivi kukaa. Kutokusafisha mikono baada ya kutoka chooni ni kitendo hatarishi kwa mhusika mwenyewe pamoja na watu anaokutana nao kwa wakati huo.
Kujenga tabia ya kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni baada ya kutoka chooni husaidia kupunguza maradhi yanayo epukika kirahisi. Kwa mujibu wa taarifa ya CDC, tendo hili huwa na faida zifuatazo-
Chanzo: CDC

- Hupunguza idadi ya watu wanaougua ugonjwa wa kuharisha kwa asilimia 23-40
- Hupunguza nafasi ya kuugua magonjwa ya mfumo wa upumuaji kwenye jamii kwa asilimia 16-21
- Hupunguza utoro wa wanafunzi shuleni unaotokana na kuugua magonjwa ya mfumo wa chakula kwa asilimia 29-57
Chanzo: CDC