Hiyo ni lugha au msemo wa kawaida sana kwenye kiswahili,hasa kwenye michezo ya watoto.katika mtaala wa kiswahili sanifu hasa fasihi simulizi kuna kipengele chenye kujumuisha hiyo michezo ya watoto kama mafunzo ya aina fulani kama yalivyo mafumbo,vitendawaili na hata ngano.
Sasa basi 'kachili saga saga' nikibwagizo katika moja ya michezo hiyo ya watoto.mfano mwimbaji au msheheleshaji wa wimbo huimba au kuanzisha kwa kusema, 'KACHILII......KACHILI...........' na hadhila yake (mara nyingi watoto wenzie katika mchezo huu) huitikia kwa kusema 'SAGA.....' huku wakipekecha viganja vyao,na mwimbaji huendelea na maneno kadha wa kadha mpaka mwisho ambapo watoto hukaa chini na kuendelea na stage(hatua) nyingine ya mchezo huu.
Lakini kutokana na upana na utajiri wa lugha yetu hii adhimu ya kiswahili maana ya mchezo na maneno ya wimbo hutegemea pia aina ya hadhila wakati wa husheheleshaji wa wimbo huo.Mfano,wakati wa kufunda mwali (unyago)wimbo huu unakua na maana nyingine kabisa lakini mara zote hua na mafundisho katika adhila hizo zote.