Sagrada Esperanca haooo kutua Dar kesho, Yanga yawasubiri

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2013
Posts
338
Reaction score
180

KIKOSI cha wachezaji 22 wa Grupo Desportivo Sagrada Esperança ya Angola kinatarajiwa kutua jijini Dar es Salaam kesho Alhamisi tayari kukabiliana na Yanga katika mechi ya kwanza ya raundi ya tatu kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Mechi hiyo inatarajiwa kupigwa katika Uwanja wa Taifa ambapo Yanga inahitaji ushindi mnono ili kuweka mazingira mazuri kabla ya kurudiana Mei 18 mjini Dundo.

Kwa habari zaidi kuhusu mpambano huo, soma hapa => Sagrada Esperanca haooo kutua Dar kesho, Yanga yawasubiri | Fikra Pevu
 
Waje tu, tuwatandike goli 3-0 mchezo uwe umeisha kabisa.
 
Waje tu, tuwatandike goli 3-0 mchezo uwe umeisha kabisa.
nafikiri wamatopeni watakua wanajiandaa kuja u/taifa kuwashangilia maana hilo ni jukumu lao walilojitwika
 
nafikiri wamatopeni watakua wanajiandaa kuja u/taifa kuwashangilia maana hilo ni jukumu lao walilojitwika
Tuwaombee tu waishi siku nyingi na pia waje kwa wingi wajionee Yanga ikifanya vitu ghali Taifa.
 
Chonde chonde baadhi ya mashabiki wachache wa simba msijitoe ufahamu safari hii mkachukua uraia wa Angola!
 
Ukimchukia mtu mwenye mafanikio unatafuta magonjwa yasiyotibika
 
hawa sagrada ndio wanavaa jezi za kijani.sasa sijui wamatopen watavaa hzo jez za kijan km kawaida yao ya kuvaa na kushangilia timu pinzan na wakimataifa,?
 
Mimi huwa sielewi kwanini mala nyingi lazima timu ngeni zianzie nyumbani kwa timu za Tz sio njia ya kuzibeba kisha timu zetu zifell tunapoenda kwao.
 
Mimi huwa sielewi kwanini mala nyingi lazima timu ngeni zianzie nyumbani kwa timu za Tz sio njia ya kuzibeba kisha timu zetu zifell tunapoenda kwao.

Huo ndio utaratibu wa FIFA wanaangalia viwango vya Soka so wewe dhaifu match zitaanzia kwako na utamalizia kwa mwenye kiwango cha juu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…