Said Kubenea: Mkataba Wa Richmond Ulisainiwa Na Lowassa Kikwete Akiwa Nje Ya Nchi

Twende kwanza na RICHMOND ambayo vifisadi vidogo vimeliibua mjengoni kumsafisha fisadi papa
 
Hapa Saed Kubenea alikuwa hajarukwa na akili
 
Kunywa maji mwanangu..hahaha...maji taka haya..hii issue nafikiri inawaumiza vichwa sana makada watiifu na wenye nia njema na chadema ...ila ndio hivyo denialism... Hili mie simo...
 
Shenzi kabisa,

ccm mko bungeni 70% na mmezunguka tz nzima mkikata viuno kuinadi ilani ya CCM yenye mahakama ya mafisadi alafu leo mnafyata mkia mnaogopa kuipeleka kesi ya Richmond kwenye mahakama ya mafisadi.
Wewe huna akili!

Wewe ni mla matapishi tu.

Ndio maana ulidekishwa barabara
 
TUNAPASWA KUSIMAMA KWENYE UKWELI.

LOWASSA NA KIKWETE NDIYO WAHUSIKA WAKUU WA RICHMOND.
PELEKA HAWA MAHAKAMA YA MAFISADI.
 
Iñashangaza kuna Leo hii mh. Lowasa ni zaidi ya wasafi classic. Tunaokumbuka kipindi kile! Dah!!.. Inchi ilisimama sejunde kadhaa, kwa nderemo na vifijo.

Tatizo Lowasa alikuwa mbabe na wenzie alikuwa anawaona kama takataka. Yeye pia alikuwa ndiyo chanzo cha: matabaka ya walio nacho na wasio nacho
 
Unaelewa maana ya mkataba?
Be serious. Serikali ya Magufuli ni ya kuendekeza mikataba ya kifisadi? Jeuri yote ya kujinasibu kunyoosha nchi ni porojo? Au ndio Waarabu wa Pemba na vilemba vyao. Mimi binafsi nasubiri kuona serikali ya Magufuli ikimchukulia hatua Lowassa na kufunga hivi vilio visivyoisha vya Richmond vinavyotupotezea mwelekeo wa Taifa. Hatuwezi kuendelea na ujinga huu huku tukijidai kuwa hakuna wasiogusika (untouchables) kwenye vita dhidi ya ufisadi. Serikali isipoweza kumfikisha Lowassa kwenye mahakama ya mafisadi basi i-"shut up" kama "mtemi" mwenyewe anavyowapasha.
 
Watanzania kuna wakati tunakuwa hopeless,hivi kwanini tusifanye mambo kisheria badala ya kusikia udaku unatolewa na mtu mwenye IQ ndogo kuliko ya bata?
Aliyetuhumiwa wakati huo na Kangaroo court ya Mwakyembe ilioshindwa kumwita Lowassa kumhoji juu ya swala hilo.
Cha ajabu wapo mazezeta kwa miaka takilibani 10 wamekuwa wakiimba Lowassa ni fisadi bila ushahidi wa kumfungulia mashtaka.
Je nani anafaidika na kupakapaka watu matope?
Acheni kutumika kama brush ya kiatu.
 
Haitakaa ije itokee Lowasa apelekwe mahakamani kwa swala la Richmond kwakua wenye mahakama(CCM) ndio wenye Richmond,hivyo ni sawa kabisa na kujipeleka jela kwa hiari yako mwenyewe.
Wanaompigia Lowasa kelele ni wale Ma MBURURA wasiojua chochote kuhusu Richmond,kwa wanaojua hawadhubutu hata kunyoosha kidole kwa Lowasa.
 
Tulishuhudia mengi sana ya ajabu na yasiyofurahisha mioyoni kipindi cha Jk, sema tu watanzania sisi ni wanafiki.
Lowasa alikuwa na makandokando mengi! Ubabe na kona kama hii nchi ipo kiganjani kwake, kiburi cha ndani kwa ndani, unafiki wa machoni na dharau ni hulka yake.
Kipindi yeye akiwa Waziri mkuu ndiyo kipindi tulichoshuhudia chanzo cha madaraja ya waliokuanacho na wasiokuanacho. Ubena mkubwa ilikuwa mwingi mno.
 
Unapoandika haya ni vema ukatuambia pia juu ya hiyo kampuni iko wapi kwa sasa na inamilikiwa na nani. Kumbuka kuwa RICHMOND ilibadilika ikawa DOWANS nayo ikabadilika ikawa SYMBION POWER ambayo ipo hadi leo na bado inaendelea kulipwa mabillion ya fedha za waTanzania je ni nani anayepokea fedha hizo kwa sasa? vipi kuhusu ESCROW unaweza kueleza lolote ni nani hasa walihusika vipi juu ya KAGODA, MEREMETA ni nani alihusika? pia usisahau kutuambia juu ya upotevu wa zaidi ya billion 250 kupitia ile Wizara aliyokuwa akiiongoza huyo unayemshabikia leo hii.
 
Mh. Kubenea ni jembe, haogopi na anajitambua. Siyo mchumia tumbo kabisa na ni msema kweli. Ubarikiwe mbunge wa ubungo kwa kuitendea haki taaluma yako kwa makala za kizalendo kama hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…