TANZIA Said Ngamba alias 'Mzee Small wa Ngamba' afariki dunia

Informer

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,606
Reaction score
6,672

Said Ngamba "Mzee Small"

Taarifa tulzozipata hivi punde kuwa muigizaji Said Ngamba au Mzee Small Amefariki dunia baada ya kuugua muda mrefu.

Mzee Small alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi kwa kipindi kirefu.

Chanzo cha taarifa hizi ni Mtoto wake wa kiume Mahmudu (Mongamba) ambaye anadai Baba yake alipelekwa hospitali ya Muhimbili Jumamosi Tar 7 Juni (jana), muda wa saa mbili asubuhi baada ya kuzidiwa. Ameeleza kwamba alishinda naye kutwa nzima ila ilipofika saa 4:09 usiku akafariki akiwa mikononi mwake.

Said Ngamba au Mzee Small (amezaliwa mw. 1955) na alikuwa msanii wa maigizo na vichekesho nchini Tanzania.

Mungu ampe pumziko jema la milele

HISTORIA YAKE FUPI

Jina lake ni Said Ngamba maarufu kwa jina la Mzee Small (58). Amezaliwa mwaka 1955. Alikuwa msanii mkongwe wa vichekesho na maigizo hapa Bongo.

Mzee Small alipata elimu ya msingi katika Shule ya Mingumbi huko Kilwa mkoani Pwani. Mbali na kuwa mkongwe, Mzee Small kila ulipozungumza naye alikuwa na kawaida ya kutamba kuwa yeye ndiye msanii wa kwanza kabisa Tanzania Bara kuchekesha runingani.

Mzee Small alianza sanaa hiyo yapata miaka 30 iliyopita na alipata kufundishwa na mwigizaji Said Seif ‘Unono' (kwa sasa na yeye ni marehemu).

Mbali na kushiriki sanaa katika vikundi mbalimbali, Mzee Small ametumika katika vikundi vya mashirika kama vile Reli, NASACO na mengine mengi, ambayo kwa sasa hayajihusishi tena na shughuli hizo.

Mzee Small alianza kujulikana sana katika fani ya uchekeshaji hasa pale alipoibuka na mchezo uliojulikana kama 50, 50, 100, na ule wa Mjini Shule uliomwelezea mwanamke wa kijijini aliyeolewa mjini.

Mbali na kutamba na michezo hiyo, Mzee Small alikuwa mcheshi na mwenye kupenda utani wakati wote, aliibuka na kichekesho kisemacho Nani Mwenye Haki, ambacho baadaye alikiboresha zaidi.

Baadaye aliibuka na kitu kingine kikali kilichokwenda kwa jina la Nani Kama Shule, huku akiwa amewashirikisha wakali wengine kama King Majuto, Kingwendu na wachekeshaji wengine wanaotamba kwa sasa Bongo.

Mzee Small ndiye alikuwa mmiliki wa kundi la sanaa linalojulikana kama Afro-Dance ambalo alilisajili mwaka 1994 kwenye Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kutoa ajira kwa vijana wa mitaani.

Pamoja na kuwa na uzoefu wa kisanaa, lakini mkongwe huyo hakuwa na mpango wa kujiunga na kundi lingine, ila alichofanya ni kurekodi na wasanii wengine alipokuwa akiitwa kwa makubaliano maalum.

Kutokana na vichekesho, Mzee Small alikuwa anatania kuwa sanaa ilimpa mke wa ndoa katika televisheni ambaye ni Bi Chau huku akianisha kuwa mkewe, Bi Fatuma alikuwa hana tatizo lolote na Bi Chau kwani alijua kinachoendelea kuwa ni kazi tu.

Mzee Small ameacha watoto watano, watatu wa kiume na wawili wa kike.

MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!

PIA SOMA
- Unamkumbuka Said Ngamba "Mzee Small" kwa yapi?
 
rip...

----------------------
PICHA ZA MATUKIO KATIKA MAZISHI

 
Mungu Aiweke pema roho ya marehemu!
 
nimepitia ukurasa wa zamaradi mketema instagram amepost pic ya mzee small kafariki
 
dah!! r.i.p mzee small.. haya sasa mbona majanga bongo muvi
 
du msani wangapi uyo anatoweka umwaka RIP mze small
 
Mmh! Kweli? Maana kazushiwa vifo vingi sana huyu mzee.
R.I.P kama kweli
 
duuu maskini...akapumzike kwa aman...
 
habari za kusikitisha ni kwamba mzee small amefariki dunia hospitalini muhimbili kwa ugonjwa wa presha.source instagram page ya zamaradi mketema na tovuti ya global publishers.
 
mzee small alikuwa anaumwa muda sana aliomba pia msaada sana wa kutibiwa, utaskia michango ikatayo changishwa sasa.r.I.p.mzee small
 
Dah another Leaders Saga

Rip.....ila huyujamaamara sita anasemewa kafa afi ngojanisubirndugu
 
Kuna taarifa nilozozipata hivi punde kuwa muigizaji Said Ngamba au Mzee Small Amefariki dunia baada ya kuugua muda mrefu.
Natanguliza pole kwa wafiwa.

unauhakika mpaka utoe RIP?

tujijengee utamaduni wa kutotoa RIP mpaka habari iwe cinfirmed... huku ndo kuchuliana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…