Mgombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Alliance for Africa Farmers Party (AAFP), Said Soud, amesema endapo atapata ridhaa ya wananchi wa Zanzibar kuwa Rais watu wanaotaka kunywa pombe watatakiwa kuwa na leseni ili kujenga nidhamu kwa Wazanzibar na kwa yule atakayekiuka atapelekwa chuo cha mafunzo kwa miezi 3.
Soud amesema hayo leo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za chama chake zilizopo Mwera, nje ya mji wa Zanzibar, wakati akitangaza azma yake ya kugombea urais kupitia Chama cha Wakulima.