Saida Kalori apata ajali mbaya Bukoba!

Saida Kalori apata ajali mbaya Bukoba!

Mathias Byabato

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2010
Posts
1,033
Reaction score
723
saida.jpg




Mwanamuziki saida kalori na mwenzake papa kishaju wamepata ajali mbaya muda mfupi ulipita katika mlima wa kashura wakati wakipita mitaani kunadi onesho lao lililotarajiwa kufanyika leo katika ukumbi wa linas club usiku wa leo.

chanzo:Gari la wazi linalomilikiwa na kampuni ya kiroyera tours lililokuwa limewabeba limeshindwa kupanda mlima na kurudi nyuma kisha kuanguka.

wote wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa kagera lakini hali ya papa kishaju inaelezwa kuwa ni mbaya

endelea kuwa JF kwa update

byabato

UPDATE
Taarifa ambazo nimepokea kutoka kwa Bw will ruta maarufu kama Will kiroyera ambaye ndiye mmiliki wa gari lililohusika na ajali na ambaye ni mmoja wa wahusika wa shoo hiyo amenieleza kwamba Saida karoli amepata majeraha kidogo na kwamba shoo ya Usiku itaendelea kama kawaida,ila papa kishaju bado huyo hospitali ya mkoa wa kagera kwa matibabu.

jioni njema
 
Warudi kumpa utukufu Mungu kwa kumwimbia Haleluya haleluya!
Pole yao pia....!
 
Miezi kadhaa iliyopita kuna watu walidai kavuta kwenye ajali...sasa sijui hii yako mkuu ina uhakika gani!
 
Muda si mrefu walisema amekufa kwenye ajali ya boti ikakanushwa. Kama ni kweli basi walianza kumchulia.
 
Inabidi atulie na kusari sana ,naona kinamtafuta.
 
Hivi yupo bado huyu mama?

yupo ,hivi sasa anafanya kazi ya studio ya TIVOL ya jijini mwanza ambapo alipanga kufanya shoo ya kukata na soka leo usiku linas na kesho mchana kaitaba,hapa bukoba kutwa nzima walikuwa wakipita na magari wakitangaza shoo hizo.
 
Miezi kadhaa iliyopita kuna watu walidai kavuta kwenye ajali...sasa sijui hii yako mkuu ina uhakika gani!

sure ths information has to be proven out behind past information relatiting to this which was then confirmed lies
 
Hata mimi nimeshangaa sana. Maana nilisoma hapa jamvini kwamba amefariki kwa ajali ya boti kuzama. Sasa hii ya leo tena imeniacha nimebaki na mshangao.

Miezi kadhaa iliyopita kuna watu walidai kavuta kwenye ajali...sasa sijui hii yako mkuu ina uhakika gani!
 
Nilishasoma taarifa zake mbili za kuzushiwa kifo huyu dada namuombea kwa mungu apone haraka!
 
CloudsFm na genge lao waharibifu sana huyu mama angekuwa mbali kama si mabaradhuli haya kumdhulumu.
 
Back
Top Bottom