Binti Msichana
Senior Member
- Oct 9, 2016
- 109
- 249
Akiongea na mtangazaji wa kituo cha redio cha Clouds , mwanamuziki mkongwe wa nyimbo za utamaduni kutoka Kagera, amemlalamikia meneja wake kumsainisha mikataba mbalimbali ya kikazi ilhali alikuwa hajui kusoma wala kuandika.
Aelezea kwa muda wa miaka 15 akiwa chini ya meneja huyu alikuwa kifungoni kwani mikataba hiyo mibaya ilimnyima hata haki ya kuongea na waandishi wa habari.
Kwa hivi sasa msanii huyo amekuja kivingine na kibao kipya kinachoitwa Olugambo.
Kwa sasa msanii huyo anajisikia huru baada ya kuachana na mkataba huo kandamizi.Julai mosi atatimiza miaka 15 katika muziki.
Ikumbukwe miaka ya nyuma msanii huyu alikuwa maarufu sana na kujizolea mashabiki wengi katika Afrika Mashariki.
Umaarufu wake na kipato chake havikuendana, kwani mikataba hiyo ilimnyonya.
Miongoni mwa nyimbo zake maarufu ni Salome iliyorudiwa na msanii Diamond.