Saida Karoli: Meneja wangu amemtapeli Diamond mamilioni, mi nilimpa wimbo bure

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2016
Posts
1,817
Reaction score
4,061
Muimbaji huyo amedai hizo asilimia 25 za mapato za wimbo ‘Salome’ ambazo zilielezwa na viongozi wa WCB hazijui kwa kuwa hakuhusishwa kwenye hilo.

“Tatizo limekuja kwa meneja wangu aliyempatia Diamond kazi, mimi nimempatia bure Diamond hiyo kazi aitumie,” alisema Saida katika runinga ya KUTV ya nchini Kenya. “Lakini kwenye kusikia masikioni kwangu na kwenye vyombo vya habari kwamba Diamond amempatia pesa milioni 25 meneja wangu wakawa wametengeneza mkataba kwamba huu wimbo utatumika hivi na hivi ila mimi kama mimi huo mkataba siujui na wala sikuuona na wala hawakunionyesha. Mimi ninachojua nimempatia kazi Diamond bure ili aitumie tuinuane wasanii wa Tanzania,”

Pia muimbaji huyo amedai yeye alishiriki kiasi fulani katika kuandaa kiitikio cha wimbo huo kwa kuingiza sauti yake.

Kaaazi kweli kweli. Kwahiyo meneja wake kachukua chake mapema
 
Huyu mama bado wanaendelea kumzurumu tu?
Kwa maelezo hayo, hakuna aliyemdhurumu. Yeye alitoa wimbo bure kwa maana ya kwamba hataki hata senti moja. Hajapewa chochote kwa kuwa hakutaka, sasa analalamika nini? Kama meneja amepewa, Saida hana haja ya kumuonea wivu. Hiyo ni facilitation fee, yaani ni malipo ya WCB kwa meneja kwa kuwezesha Saida atoe wimbo bure. Kwenye mkataba, kila mtu anapata alichokubaliana nacho
 
Kweli meneja ana roho anaitwa nani huyo meneja zulmati tumuanike. Mi mwenyewe nilifurahi at least Saida kapata tupesa
 
Muimbaji huyo amedai hizo asilimia 25 za mapato za wimbo ‘Salome’ ambazo zilielezwa na viongozi wa WCB hazijui kwa kuwa hakuhusishwa kwenye hilo.

“Tatizo limekuja kwa meneja wangu aliyempatia Diamond kazi, mimi nimempatia bure Diamond hiyo kazi aitumie,” alisema Saida katika runinga ya KUTV ya nchini Kenya. “Lakini kwenye kusikia masikioni kwangu na kwenye vyombo vya habari kwamba Diamond amempatia pesa milioni 25 meneja wangu wakawa wametengeneza mkataba kwamba huu wimbo utatumika hivi na hivi ila mimi kama mimi huo mkataba siujui na wala sikuuona na wala hawakunionyesha. Mimi ninachojua nimempatia kazi Diamond bure ili aitumie tuinuane wasanii wa Tanzania,”

Pia muimbaji huyo amedai yeye alishiriki kiasi fulani katika kuandaa kiitikio cha wimbo huo kwa kuingiza sauti yake.

Muta na Ruge Mutahaba ni ndugu?
 
Back
Top Bottom