Mfanyabiashara Saidi Lugumi ( @lugumisaidi ) hapo jana November 23 ameendeleza utamaduni wake wa kusaidia Watu wenye mahitaji kwa kujumuika na Watoto yatima wa Vituo vitano nyumbani kwake Masaki Dar es salaam ambapo awamu hii amewakusanya zaidi ya Watoto 700 na kufanya ibada, kula, kunywa na kucheza pamoja kwa siku nzima.
Lugumi ambaye amekuwa akisaidia Watoto yatima katika vituo mbalimbali toka mwaka 2013 ( miaka 11 iliyopita) amekuwa akiwahudumia Watoto hao kwa miaka mingi ikiwa ni pamoja na kuajiri Madaktari wanaowahudumia, kuwanunulia umeme, kuwalipia maji, kuwafanyia ‘shopping’ ya nguo kila baada ya miezi mitatu, kuwapelekea chakula kila mwisho wa mwezi, kuwasomesha hadi Vyuo Vikuu na kuwatafutia kazi.
“Kila kituo kina Afisa Ustawi wa Jamii, kila kituo tumepeleka Mabasi (Coaster) kama mchango wetu ili Watoto wawe wanaweza kupelekwa shuleni, hatufanyi hivi kwa kutaka sifa hapana.... sisi tunafanya kwa mujibu wa Quran, unajua sisi dini ya Kiislamu imetuamrisha ni lazima Muislamu mwenye uwezo lazima awasaidie hawa Watoto” - amesema Saidi Lugumi.
“Mimi nimezaliwa Magu, Mwanza tulizaliwa Watoto zaidi ya 16, mimi nimesoma mpaka darasa la saba na Mungu akajalia, hili jambo linawasumbua Watu.. kila Mwanadamu unaemuona wewe amejaliwa riziki yake, alichokipanga Mungu kwangu kitakuwa..... wewe kasirika, nuna, fanya unavyofanya lakini siku ya Mungu aliyotaka lazima itakuwa, kwahiyo Mungu huyuhuyu akatuamrisha sisi tuweze kuwa na hawa Watoto, tunafanya biashara sisi sio wezi, hatujawahi kumtapeli Mtu, hatujawahi kumfitini Mtu na hatutegemei....”
“Sisi tukiwa na ziki yetu tutakaa na ziki yetu na Watoto wetu, huwa tunakwama nakumbuka kipindi cha nyuma tulikwama tukatoka kwenye kula nyama, kuku, mayai.... tukawa tunakula kila siku dagaa maharage, Kikwete kanisaidia sana, Mama Samia kanisaidia sana, kuna wakati sisi tunakwama vyakula hapa tunakuwa hatuna hela tukiomba hela nje zikichelewa tunamuomba huyu Mama, kuna muda sina hela mambo yamekuwa magumu, ni kawaida” - Said Lugumi