Wana JF wenye blogu tupo wengi sana, sema sasa katika blogu zetu tunatumia majina halisi, anuani halisi, barua pepe na namba za simu, tofauti na hapa JF. Sasa tukisema tukupatie viungo vya blogu zetu kwa sisi wengine itakuwa mshike mshike na sirikali, hasa sisi wakosoaji. Kwa ujumla JF ina 'reputation' mbaya sana sirikalini na tunaogopwa sana.
Hii itatufanya tusiwe huru sana mitaani, kwani huenda maisha yetu binafsi yatachunguzwa na wasioitakia JF maendeleo.
Kwa mimi ni hayo tu.