Saidia: Mtoto Anna Munyasa (miaka 5) Amepotea - Anatafutwa na mama yake.

Steve Dii

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2007
Posts
6,402
Reaction score
1,273
Wakuu,

Nimepokea ujumbe kuhusiana na kupotea kwa mtoto ANNA MUNYASA huko Uingereza. Nimefanya search kwenye net kuangalia kama kuna habari zozote zilizoandikwa na kama kuna detailed information zozote kusaidia wasamaria wema kumsadia mama mzazi anayemtafuta mtoto wake ampate.

Mtoto amepotea Uingereza tangu July mwaka huu. Inawezekana/inasemekana baba mzazi, REMIGIUS MUNYASA amemtoroshea mtoto na kumleta huku Tanzania, lakini habari hii haina uhakika sana. Police wa hapa Bongo kama nilivyosoma habari ya BBC naona wameshajulishwa. Pia vyombo mbalimbali (border control) vimeshajulishwa.

Picha za mtoto Anna Munyasa


Source: BBC


Source: Helpfindmychild.net


Picha ya mama mzazi, Rosemary Kimolo


Source: BBC


Picha ya baba mzazi, Remigius Munyasa


Source: Helpmefindmychild.net


Kwa wenye ufahamu mtoto huyu alipo, tafadhali sana wasiliana na Police hapa Tanzania.
Kwa walioko Uingereza na popote pengine pale wanaweza pia kuwasilisha habari kwa: West Midlands Police - (+44) 845-113 5000 au NPIA Missing Persons Bureau on (+44) 808-100 8777. Pia unaweza kutembelea mtandao huu http://www.helpfindmychild.net/anna-munyasa kupata maelezo zaidi na kuweza kutuma barua pepe hapa.

Shukrani.


SteveD.
 
ASANTE KWA TAARIFA TUTAJITAHIDI KUSAIDIA MALA TU TUTaKAPO PATA INFORMATION YOYOTE JUU YA HUYU MTOTO MZURI

mama wa mtoto omba na kuamini mtoto wako utampata salama kwa uwezo wa mungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…