Kiungo Mshambuliaji wa Simba Saido Ntibazonkiza ambaye jana amefunga mabao 5 peke yake na kuwafanya Yanga washtuke na kumsafirisha jijini Mbeya kwa ajili ya mchezo wa mwisho dhidi ya Prisons, ni mchezaji muhimu sana katika kikosi cha Simba chini ya huyu kocha Mbrazil.
Nyie fuatilieni mtaamini, Robertinho anavutiwa sana na style ya uchezaji ya Mrundi huyo. Robertinho anamuona Saido ana msaada mno kuliko mchezaji yeyote wa Simba akiwemo Triple C.
Huwezi kumuona kocha anamtoa kizembe zembe Ntibazonkiza, mechi zote kubwa Saido kamaliza, kwahiyo wale wanaopinga kuwa Saido hawezi kufunga mabao 5 mechi moja ni wajinga tu.