Saidoo wetu ndiye anawabeba kwasasa

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Hali ni tete waungwana huko upande wa pili, siku mbili hizi zimekuwepo tambo za kufa mtu toka kwa msemaji tukajua baada ya Cska Moscow Mbeya City wangekula 8.

Hatimaye hatukuamini tulichokiona jana kwa Mkapa. Waliotuahidi pira Dubai waliomba mpira uishe zilipofika dakika ya 75. Hali si hali.

Kiuhalisia ukiondoa penati ile ya 'zawadi' na red card mkubwa alikua anaumbuka mapema.

Kikubwa pongezi kubwa kwa kijana wetu Ntibazokiza kwa kuwastiri hawa jirani na amewaokia tokea mechi ya mwanzo siku ile alioanza, hakika kwa sasa yeye ndiye amekuja kuwa mwokozi wa timu maana tunaona sasa hata yule ccc first half hamalizi anaenda kusugua!

Pongezi kubwa wananchi kwa kuwa na scout nzuri, kuwa na watu mahiri ambao hata wakitoka wanasaidia sana timu nyingine.

Inshallah msimu ujao hebu tumfungulie milengo fundi saidoo arudi jangwani,kama tumeweza kumpokea Metacha kwanini isiwe kwa Ntibazokiza?

#Bring back our Saidoo
 
Hakika aliewaita utopolo aliwaza mbali sana
 
Mtaita maji mmaaa na anakiwasha hajawahi kukiwasha hivi akiwa utopoloni...
 
Kweli huko Yanga hakuna mwenye akili hata mmoja,yaani Saido Ntibazonkiza leo hii ni mchezaji wa Utopolo? Bora kukosa mali kuliko kukosa akili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…