Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Ni siku nyingine tena tupitie mambo ambayo hutufanya tujifunze namna ya kuishi na kuwa bora zaidi
Fahamu kwamba kama watu hawa kupendi basi jua unafanya mambo yako kwa usahihi,si unajua kuna ile mambo ya shule unasoma sana na kujituma utaambiwa "huyu nae anasomea kijiji" au unafanya kazi zako kwa bidii na kujituma utasikia "huyu nae kama boss ndugu yake
Kaa mbali na ugomvi wa wanandoa au wapenzi,kwasababu wanaweza kupatana mara moja,halafu kwako ikawa aibu
Fahamu kwamba usitegemee watu wafanye mambo ambayo wewe mwenyewe huwezi kufanya
Jiangalie wewe binafsi kwanza kabla huja wajaji watu wengine,jifanyie tathimini kwanza wewe binafsi halafu ndio uwe na jeuri ya kuwaongelea wengine
Siku zote usifikirie kwamba wewe una akili sana au mwerevu sana kupita watu wengine
Siku zote endelea kujifunza na kukua ili moyo wako uendelee kuwa mzuri
Hauwezi kuamua nani umpende ila unaweza kuhimili matokeo ya kumpenda mtu huyo
Ni hayo tu!