SAIKOLOJIA: Kanini Mwandiko Una Jinsia ya Kike na ya Kiume? Maajabu!

Joined
Jul 28, 2013
Posts
72
Reaction score
17
Inawezeka wengi walishajiuliza kwanini, kunamwandiko wa kiume na wakike! Jinsia katika mwandiko inatoka wapi? Kwanini mwandiko wa kike unatofautiana na wa kiume?

katika utafiti ulifanywa na wanasaikolijia imeonyesha kuwa mwandiko wa kike huathriwa na mambo yafuatayo:-

1. kunahomoni amabazo huathiri mwandiko wao kwa ujumla

2. Kuna mahusiano makubwa sana kati ya mwandiko wa kike na akili au uwezo wa kufikiria kwa mwanamke. Tafiti zimeonyesha kuwa mwanamke hufikiria sana kwa kila jambo na huwa mzito wa kutoa maamuzi yake. Tabia hii pia huathiri namna ya uumbaji wa herufi zake. jambo hili ni tofauti kwa wanaume.

3. kila mwanamke anataka kufanya jambo lolote kwa dhana ya bila kukosea yaani kwa usahihi zaidi ( free of error notions). Jambo hili ndilo linalowafanya kuchelewa kutoa maazuzi.

4.Mengineyo katika saikolijia ya mwanamke:

mwanamke hufurahia zaidi kuliko mwanamke akisifiwa! Siku zote mwanamke anapenda kuwa mbele katika jamii zao, mwanamke anapenda kubemelezwa zaidi kuliko hata mtoto....


JARIBIO: Chunguza muda wa mtoto wa kike kujiandaa kwenda kazini, out na kadhalika , utagundua kuwa ni karibia mara mbili ya muda wa mtoto wa kiume!
 
nafikiri kuna point hapo mkuu though sina uhakika kivileeeeeeeeeeee
 
dah! nilikua nasoma nikim-refer mtu fulani.
 
Mkuu Mwalimu Tanzania,

Ingawaje kuna uhusiano na pengine ukweli katika baadhi ya uyasemayo hapo juu, nina maswali machache,

1. Ni vichochezi (hormones) gani zilizogunduliwa kuhusishwa na utafiti huu/huo?

2. Uhusiano kati ya akili na mwandiko ni upi, kwani kana kwa kuegemea uhusiano huu ningetegemea kuwa wengi wa wanawake hawa wenye miandiko mizuri wawe na 'akili nyingi' bright/smart/brilliant! (No offence).
 
Last edited by a moderator:
Kweli akili ni nywele kila mmoja ana zake...hao ndo watu wenye akili si kila mtu abane suruali na kuvaa miwani mikubwa wengine wanatakiwa kubaki waumize vichwa kwa kila kitu kujiuliza kwa nini?
 
 
Wazazi wetu waliosoma enzi za mkoloni walikuwa na miandiko inayofanana kati ya me na ke, hata Waingereza mpaka leo- hivi hii pia inahusu mada yako?
 
La haula!

Mimi ni mwanamme na bumla wa mwisho!

Duh!
 
c.c Mwalimu Tanzania
2. Kuna mahusiano makubwa sana kati ya mwandiko wa kike na akili au uwezo wa kufikiria kwa mwanamke. Tafiti zimeonyesha kuwa mwanamke hufikiria sana kwa kila jambo na huwa mzito wa kutoa maamuzi yake. Tabia hii pia huathiri namna ya uumbaji wa herufi zake. jambo hili ni tofauti kwa wanaume.

Kuna uhusiano wowote kati ya kuumba herufi na kufikir! Je, ndio kusema na wanaume wanaoumba herufi vizuri na wenyewe wanauwezo mkubwa wa kufikiri? Mbona wanaume wengi wenye miandiko mibaya ndio wanaofikiri vizuri! Je, wanawake wanaoumba herufi vibaya uwezo wao wa kufikir ni mdogo? Je, kisaikolojia akili na kufikiri ni kitu kimoja?


4.Mengineyo katika saikolijia ya mwanamke:

mwanamke hufurahia zaidi kuliko mwanamke akisifiwa!
Siku zote mwanamke anapenda kuwa mbele katika jamii zao,
Nimeshindwa kuelewa kwenye red. kwenye blue wanawake wa kizungu tu au hata wa Kiafrika? Maana wengi hapa mjini hawajiamini na huko vijijini ndio balaaa...!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…