Saikolojia nyepesi tambua maana ya maneno ambayo mke wako hutumia kukulegeza hadi kuhofu

venchwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2016
Posts
1,677
Reaction score
1,596
SAIKOLOJIA NYEPESI
TAMBUA MAANA YA MANENO AMBAYO MKE WAKO HUTUMIA.
1. "Sawa bwana" (fine). Hutumiwa na mke kumaliza mabishano nawe. Akisema hivyo ujue anahitaji unyamaze.
2. "Dakika tano tu" (five minutes only) Akisema nipe dakika tano wakati unatoka naye maana yake ni nusu saa, ila dakika tano huwa dakika tano kweli kama akikwambia wewe ndani ya dakika tano uwe umerudi nyumbani.
3. "Hamna kitu" (Nothing)Humaanisha ni utulivu wa muda, maswali zaidi yataleta mabishano makubwa.
4. "Endelea tu na mambo yako" (Go Ahead) Anamaanisha "jaribu uone" sio ruhusa ya kukuruhusu uendelee kufanya jambo hilo.
5. "Kushusha pumzi kwa nguvu" (loud sigh) Ni kitendo kinachomaanisha kwamba wewe ni mpumbavu na anapoteza muda wake kubishana na wewe juu ya upumbavu uliofanya.
6. "Hamna tatizo" (that's okay) Huonyesha kuna makosa fulani na kwamba anataka ufikiri zaidi kabla hajaamua kutenda.
7. "Asante" (thank you) Mke akikwambia Asante, wewe mjibu tu "karibu" ina maana kafurahi, ila kama akikwambia "Asante sana" ujue kuna kitu umemuudhi.
8. "Fanya utakalo" (whatever). Ni njia ya kukwambia nenda zako, haunibabaishi (go to hell!!)
9. "Usihofu kuhusu hilo, nimeshaelewa". (Worry not, i know) Ni sentensi tata kutoka kwa mke inayomaanisha wewe siyo mtekelezaji wa ahadi zako.
10. Ni ukweli kwamba mwanamke ni vigumu sana kumuelewa , ila vyovyote vile alivyo, mke ni uumbaji bora kabisa wa Mungu alioufanya. Kuwa na mke ndani ya nyumba huleta utulivu wa nafsi! Mwanzo 2:23 -25
Keep Smiling ..
 
Yote ulosema yanakaribiana na ukweli ila hapo kwenye bold umekosea! Mwanamke hakuumbwa, mwanamke sio mwana-Adamu, mwanamke ni mwanamke tu kama alivyo, ni kiumbe dhaifu kinachotumiwa na shetani kuangamiza mipango ya Mungu wa kweli.
Adui mpende - Mwanamke mpende, nafikiri nimesomeka vyema. Najua wanawake watanielewa ndivyo sivyo, ila ukweli ndio huo.
 
Nimekuwa nikiyasikia kwa mpenzi wangu ila tafsiri yake sikuwa naijua.Leo nimeelewa.
 
Hii saikoloji nzuri mno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…