SoC01 Saikolojia ya kujiamini na faida zake kwa binadamu

Stories of Change - 2021 Competition
Joined
Jul 15, 2021
Posts
16
Reaction score
61
Kila mwanadamu ana nafsi (self) ya kipekee ambayo inahitaji mazingira chanya na msukumo wa ndani (internal will) ili kukuwa. Wengi wetu hatuthamini msukumo wa ndani kwenye ukuaji wa nafsi zetu bali tunathamini sana mazingira yetu kama kichocheo namba moja cha ukuwaji wa nafsi zetu. Kwa mtizamo huu kisanyansi sio sahihi na itapelekea nafsi zetu ama uwezo wetu kufa na kupelekea kushindwa kufanikiwa kwa kiwango tunachohitaji kama wanadamu.

Kama ilivyo vinasaba (DNA) ilivyo ya kipekee kwa kila mwanadamu ndivyo hivyo hivyo ilivyo nafsi. Kila mwanadamu ana nafsi ya kipekee na kila mtu anauwezo wa kuiongoza nafsi yake kwa kuipa vichocheo chanya kwa ukuaji sahihi wa nafsi ili kuleta mafanikio kwa kila kitu mwanadamu anachofanya. Pindi nafsi yako inapokufa ni dhahiri mafanikio yako yatakuwa kwa uchache sana ama kutokufanikiwa kabisa.

Namna pekee ya kuipa afya njema nafsi yako ni kwa kutumia kichocheo chanya kiitwacho kujiamini. Wengi wetu tunadharau sana kichocheo hichi cha kujiamini tukidhani hakina umuhimu na hivyo tukiishi kwa mategemeo ya vichocheo vitokanavyo na mazingira yetu ambayo mengi huwa ni hasi katika ukuaji wa nafsi zetu.

Kamusi ya saikolojia inafasili kujiamini kama imani binafsi ya mtu kwenye uwezo wake, jitihada na maamuzi au imani itakayomuwezesha mtu kuweza kukabiliana na changamoto ya mazingira na mahitaji yake kikamilifu.

Kusisitiza umuhimu wa kujiamini, mwanasaikolojia Nathaniel Branden kwenye kitabu chake kitwacho Saikolojia ya Kujithamini cha mwaka 1969 amehimiza ya kuwa matatizo mengi ya akili na hisia yanayowasibu watu chanzo chake ni kutokujiamini. Zaidi ya yote, Nathaniel Branden amesema kuboresha kichocheo cha kujiamini kunaleta matokeo chanya na hata kutibu magonjwa.

Badala ya kwenda kwa kina katika nadharia mbalimbli za kisayansi juu ya kichocheo cha kujiamini sasa tuangalie uhalisia wa namna tunavyoua nafsi zetu na namna ambayo tunaweza kuboresha nafsi zetu.

Kila kitu tunachokifanya katika maisha yetu ni matokeo ya nafsi imara ambayo kichocheo chake kikuu ni msukumo wetu wa ndani na kwa kiwango kidogo sana mazingira. Kosa kubwa tunalolifanya ni kutegemea mazingira yetu kuboresha nafsi yetu na ama kutuaminisha ya kuwa tunaweza kufanya jambo. Uwezo wa mtu kutenda jambo linaanza ndani mwako na wewe binafsi unapaswa kujua, kuaelewa na kuamini kuwa unaweza kufanya na hapo ndipo kujiamini kunapoanza.

Tuangalie mifano kidogo, ukiwa mwanasoka imani inapaswa kuanza na wewe kuwa unauwezo wa kucheza mpira, kuweka jitihada na kuamini kuwa utaweza, kutafuta shehemu sahihi za kufikisha ndoto zako na bila kukata taamaa. Ila ukweli ni kinyume chake, wanasokoa wengi kwanza huanza kwa kusikiliza maoni ya watu juu ya uwezo wao, wanataka watu ndio wathibitishe ubora wao au kukataa uwezo ama ubora wao na wengi wao baada ya kukataliwa na watu huishia hapo na ndoto hufia hapo na kuanza kufanya kitu kingine. Kwa mfano huu mdogo, hivi ndivyo wengi wetu tulivyo katika maisha yetu, tunategemea msukumo chanya (positive reinforcement) kutoka kwenye jamii ili kutenda jambo na jamii isipokubali basi tunakata tamaa na kuacha kabisa.

Sisemi jamii sio muhimu katika ukuaji wa nafsi, la hasha! Ila mazingira chanya ni machache sana kwenye ukuaji wa nafsi. Ili jamii na mazingira yako yanayokuzunguka yaweze kuthibitisha uwezo wako ni mpaka imani yako na kujiamini kwako kuanze kuonyesha uwezo wako kwa jamii ndipo jamii wakubali au wakatae. Hivyo kuiamini nafsi yako ndio kitu muhimu sana kabla ya jamii kukubali au kuelewa uwezo wako. Jamii haiwezi kuelewa uwezo wako kabla ya wewe mwenyewe kujiamini na kuamini kile unachokifanya.

Katika ulimwengu wa leo, kuna watu wachache sana waliofanikiwa na ni ukweli kuwa wamechagua kujiamini na kuipa vichocheo chanya nafsi zao kisha wakaenda kufanya mambo makubwa sana ambayo yanabaki kuishangaza jamii. Watu hawa wengi ukifuatilia historia za maisha yao utaona kabisa jamii na mazingira yao yaliwakataa na kuwaambia hawawezi kufanikiwa ila kujiamini kwao kukafanya nafsi zao kuwa imara na mwisho wa siku kufanya mambo makubwa sana kutokana na kile walichokiamini.

Ili kuleta mafanikio katika maisha yako na kuboresha afya ya mwili na nafsi yako fanya kile unachokiamini, unachokiweza kwa kujiamini hata kama jamii yako itakwambia haiwezekani, hakuna mtu aliwahi kufanikiwa, hautafanikiwa na mengine mengi. Nafsi yako ni kama ua linalokuwa kwa kuwekwa mbolea na maji, pindi unapoacha tu kuipa nafsi yako kichocheo cha kujiamini hapo huanza kusinyaa na itakubaliana na mazingira yako kuwa huwezi na kukufanya kushindwa kufanikiwa katika maisha yako.

Ukitaka kuona ni kwa namna gani nafsi yako imeanza kufa kwa kukosa kujiamini na kutegemea imani ya mazingira yako angalia vile mitandao ya kijamii imetugeuza mazuzu leo. Kila unachofanya unaweka kwenye mtandao ili upate mrejesho kutoka kwa jamii yako na mara zote unategemea kupata mrejesho chanya na mara tu unapopata mrejesho hasi unakuwa na msongo wa mawazo na kuanza kuangaika kutafuta njia za wewe kukubalika kwenye jamii na sio wewe binafsi kujikubali. Tizama vile watu ambavyo hujionyesha sura zao, maumbo yao, chakula chao, starehe zao, nguo zao kila siku ama kila muda kwenye mitandao ya jamii hii ni ishara tosha watu hawa hawajiamini na nafsi zao zimeanza kufa. Kukosa imani na nafsi yako ni ugonjwa wa kisaikoljia japo wengi wetu hatudhani kama ni ugonjwa ila tunaona ni usasa na bila kufanya hivyo tunaonekana tuko nyuma ya wakati.

Mtu mwenye nafsi hai na mwenye kujiamini ni yule ambae anafanya jambo kwa faida yake litokanalo na kujiamini hivyo haihitaji ridhaa ya jamii yako kwa kile unachokifanya. Kama mtu umeumbwa mrembo na wewe unajua hivyo haihitaji tena ridhaa ya watu wengine kukuonyesha kuwa wewe ni mzuri. Matokeo ya kutojiamini ni kuanza kujionyesha kuwa ni mrembo kwa matakwa ya jamii kwa kuanza kuvaa mavazi wanayoafiki jamii, kuanza kupaka vipodozi wanavyokubali jamii, kwenda sehemu wanazokubali jamii hata kama wewe hupendi unajikuta unafanya kwa matakwa ya jamii ila sio kwa imani yako.

Anza kujiamini na kuboresha afya ya nafsi yako kwa faida yako kwa kuanza kufanya mambo unayoyaamini wewe binafsi na sio jamii yako, kufanya mambo unayoyaweza na kuyamudu, kufanya mambo yenye kukuletea faida wewe binafsi na sio jamii na mwisho kuamini uwezo wako binafsi kwanza kabla ya kukatishwa tamaa na jamii yako. Namna bora ya kufufua nafsi yako ni kwa kuanza kujifunza vizuri kuhusu wewe, uwezo wako, nguvu yako, kipaji chako, uzuri wako na mchango wako kwa jamii. Kisha, anza kujiamini na kutenda yale tu unayoyaamini bila kuangalia jamii inasema nini maana jamii inapaswa kuona matokeo ya nafsi yako na kuyasadiki hivyo kiongozi wa nafsi yako ni amani yako wewe mweneyewe kwako.
 
Upvote 12

Approved. Hongera sana.
 
Iko poaa
 
Back
Top Bottom