Saikolojia ya maisha njia ya kutafuta na kupata kazi kiurahisi

Saikolojia ya maisha njia ya kutafuta na kupata kazi kiurahisi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Njia ya kutafuta na kupata kazi kirahisi


Kuishi muda mrefu bila kuwa na kazi kuna madhara mengi kisaikolojia, watu wengi hupatwa na vichaa na wengine, kujiingiza katika ulevi wa kupindukia, utumiaji dawa za kulevya na uhuni kutokana na kukata tamaa ya maisha hasa wanapopoteza kazi au wanapomaliza masomo na kukosa ajira walizokuwa wakizitazamia.

Hii inatokana na watu wengi kukosa elimu ya namna ya wanavyoweza kutumia vizuri muda wao wa dhahabu wanapokuwa hawana kazi. Unaitwa muda wa dhahabu au ‘Unemployment golden time’ kwa sababu mkosa ajira huathirika endapo atashindwa kutumia muda wa awali kujiokoa na makucha ya kukosa kazi.

Wataalamu wa masuala ya ndege wanaziita sekunde 90 za awali baada ya ndege kuanguka kuwa ni “golden time” kwa sababu ndizo ambazo mtu anaweza kuzitumia kujiokoa, vinginevyo hali huwa mbaya na pengine kuna uwezekano mdogo wa wahanga kutoka salama baada ya dakika hizo kupita.

Hivyo basi maisha bila ajira nayo yana muda wake ‘golden time.’ Ni rahisi kupata kazi muda mfupi baada ya kumaliza shule au kufukuzwa kazi kuliko kukaa nje ya ajira (kijiweni) kwa miaka sita au saba.

Kimsingi kuna maangalizo mengi katika mada hii ambayo watu wasiokuwa na ajira wanatakiwa kuzingatia lakini kwa uchache tutaangalia yale ambayo ni muhimu kufuatwa na watafuta ajira ili waweze kutumia ‘golden time’ vizuri na kuweza kuepuka madhara ya kisaikolojia na kutopata kazi.

KUTOTAHARUKI
Inashauriwa kuwa muda mfupi baada ya kufutwa kazi au kumaliza masomo na kukutana na vikwazo vya awali vya kukosa kazi, mhusika hatakiwi kuwa na taharuki kwa kuanza kunywa pombe, kustarehe, kuwa na msongo wa mawazo, bali anatakiwa kutulia na kuendelea kushikamana na wafanyakazi wenzake wa awali, wanafunzi waliomaliza naye shule na watu ambao wako kwenye mtandao wa kazi, ili kujiweka katika mazingira ya kuokoka ndani ya muda muafaka.

KUJITAMBUA
Mkosa ajira anatakiwa kujitambua kuwa yeye ni nani na kuhakikisha kuwa maisha yake yanakwenda kama yeye alivyo. Mhusika anatakiwa kutunza kumbukumbu zote za elimu yake kama vyeti na kuwa hai kila siku katika ujuzi wake. Pia haifai kuwa na aibu kwa kujiona duni, ni vema kuwa na imani kuwa kipindi cha kukosa ajira ni cha muda mfupi.

KUJITAMBULISHA
Muda wa awali ambao mtu atakuwa hana kazi ni muhimu sana kwake kufanya utambulisho kwa rafiki zake, ahakikishe kuwa watu wanaweza kuwasiliana naye kwa urahisi. Si busara kujifungia chumbani na kufunga simu, kufanya hivyo kunaweza kuwafanya rafiki zako washindwe kukupa dokezo za nafasi za kazi na hata kukusahau kabisa.

KUWA TAYARI
Unapokuwa katika ‘unemployment golden time’ni lazima uwe tayari wakati wote kwa kuanza kazi, isiwe unaambiwa kazi imepatikana unaanza kusema “sina vyeti, viko kwa bibi” muda wa dhahabu lazima utumike vizuri ili kutopoteza muda wa kujikomboa. Ni muhimu pia kuandaa CV yako na kuwa nayo kwenye kabati ili itakapohitajika usipoteze muda kuiandaa!

USIULEMAZE MWILI
Kuna watu ambao huchelewa kuamka au kushinda wamelala kwa sababu hawana kazi za kufanya, jambo ambalo ni hatari kwa afya. Hata kama ukosefu wa ajira unakuumiza kiasi gani usikubali kubweteka kwa kulala, utumikishe mwili pengine hata kwa kazi ambazo si za masilahi makubwa. Haifai kulazimisha sana ajira kwa kuwaganda mabosi.

USIKATE TAMAA
Kifupi hatua hizi ni muongozo wa kuweza kutumia muda wa dhahabu katika kupata kazi, hata hivyo mtu hatakiwi kukata tamaa ya kutafuta kazi ingawa ukweli utabaki kuwa kadiri unavyozidi kuchelewa kupata kazi kwa miaka mingi ndivyo anavyozidi kuweka mazingira magumu ya kuajiriwa. Hivyo ni bora ukahangaika mapema kwa kutumia uwezo na mbinu zote ili kuepuka kupotea katika ulimwengu wa ajira na kujikuta umeathirika kisaikolojia.

 
mmmh mkuu naona ni dalili kama za magonjwa ya ukimwi , ushauri nasaha ila ku dead kuko pale pale
 
Kiongozi MziziMkavu, Mafundisho uliyoyatoa yamenigusa kiroho na kimwili! Kwa kutotaharuki baada ya kutokuwa na kazi na kuendelea kushikamana na waliokuwa wafanyanyakazi wenzangu,japo wengine wenda ndiyo waliochangia kufukuzwa kwangu kazi,nitakuwa nadumisha amri kuu kuliko zote ambayo ni "UPENDO." Na kimwili ni kwa kutokuulemaza mwili kwa kulala na kuchelewa kuamka eti kwa sababu sina kazi kwani riziki ya mbwa ipo miguuni mwake!
 
mmmh mkuu naona ni dalili kama za magonjwa ya ukimwi , ushauri nasaha ila ku dead kuko pale pale

Pole sana endelea kutumia ARV's. Kudead kila mtu hata asiye na maambukizi ya ukimwi kama wewe atadead tu.Zingatia sana ushauri wa daktari.Ukitaka tiba mbadara wasiliana na mkuu MziziMkavu.
 
mmmh mkuu naona ni dalili kama za magonjwa ya ukimwi , ushauri nasaha ila ku dead kuko pale pale
Mkuu uvugizi Kama unao ugonjwa wa Ukimwi pole sana Fuata ushauri wangu hapo chini huenda ukakusaidia inshallah.

  • LISHE YA KUONGEZA KINGA MWILINI NA CD4‏

    Virusi vya ukimwi ( V.V.U. ) hudhoofisha nguvu za mwili
    kujikinga na maradhi nyemelezi. Mgonjwa hushambuliwa na
    maradhi kwa sababu kinga mwilini imepungua. Lishe ya kuongeza
    CD4 husaidia kuongeza kinga mwilini na kupunguza makali ya
    ukimwi.

    ZINGATIA;
    Siyo watu wote wenye maambukizi ya ukimwi wanalazimika kuanza

    kutumia lishe ya kuongeza CD4 na kupunguza makali ya ukimwi.

    Utaanza tu kutumia kwa kutegemea hali ya afya yako, idadi ya
    chembechembe za CD4..

    LISHE NA DAWA ZA KUONGEZA CD4 NI NINI ?

    Ni dawa zenye uwezo wa kupunguza makali ya V.V.U

    mwilini.Huongeza kinga mwilini na kumpa mgonjwa nafuu kwa kumpa

    nguvu ya kufanya shughuli zake kama kawaida.

    Ikiwa kinga itapungua sana na kuanza kushambuliwa mara kwa mara na

    maradhi nyemelezi, unashauriwa uanze kutumia lishe ya CD4.

    LISHE YA KUONGEZA KINGA MWILINI.
    Kwa ajili ya kuongeza kinga mwilini tumia moja ya fomula nne za hapa chini:

    CD4 Fomula 1

    Vitu vinavyohitajika:

    Mbegu za figili (unga) - kijiko kimoja cha chakula.

    Haba Soda (unga) - kijiko kimoja cha chakula.

    Kitunguu thaumu (unga) - kijiko kimoja cha chakula.

    Asali Safi ya nyuki - lita moja

    Sufa - kijiko kimoja cha chakula.


    Mdalasini (unga) - kijiko kimoja cha chakula.
    Matayarisho: Vitu vyote hivyo vichanganywe pamoja hadi viwe juisi.
    Matumizi: Kunywa vijiko vitatu vya chakula kutwa mara tatu.

    CD4 Additive Fomula 2:
    Vitu vinavyohitajika:

    Karoti 2
    Ndizi mbivu 2
    Pilipili mboga 2
    Chumvi kidogo
    Ndimu 1
    Nanasi robo kilo
    Njegere robo kilo
    Kunde mbichi robo kilo
    Papai bichi 1
    Karanga robo kilo
    Embe kubwa 1
    Parachichi 1

    Matayarisho:
    Vitu vyote hivyo visagwe pamoja hadi viwe juisi.

    Matumizi: Kunywa glass moja kutwa mara mbili.

    CD4 Additive Fomula 3

    Vitu vinavyohitajika:
    Karoti iliyosagwa robo kilo.
    Kitunguu thaumu (unga) robo kilo.
    Mdalasini wa unga robo kilo.
    Tangawizi ya unga robo kilo.
    Majani ya Alovera matatu (yasagwe).
    Asali lita moja.
    Limau 2

    Matayarisho: Ongeza maji lita mbili na uache kwa muda wa masaa 8 kisha chuja na uhifadhi
    kwenye friji.
    Matumizi:
    Kikombe cha kahawa kutwa mara 4 kwa muda wa mwezi mmoja.

    CD4 Additive Fomula 4
    Vitu vinavyohitajika:
    Tende 1kg.

    Kitunguu thaumu robo kilo.
    Maziwa halisi 1 lita.
    Uwatu vijiko vikubwa vinne.
    Mdalsini (unga) vijiko vikubwa vinne.
    Tangawizi ya unga vijiko vikubwa vinne.
    Haba Soda ya unga vijiko vikubwa vinne.

    Matayarisho:
    Saga tende na maziwa kwa pamoja kisha changanya vitu vingine na weka jikoni na kuvipika
    pamoja hadi viive.

    Matumizi:
    Kula vijiko viwili vikubwa (vya chakula) mara tatu kwa siku kwa muda wa miezi mitatu.
    Zingatia: Baadhi ya vitu vilivyotajwa hapo juu vinapatikana kwenye maduka ya dawa za
    Kisunnah na Kiarabu, hivyo ni muhimu kuvipata kutoka kwenye maduka halisi yanayouza vitu
    hivyo.

    Aidha kwa wale ambao hawawezi kujitengenezea wenyewe dawa hizi, wakumbuke kwamba
    tunayo dawa ya AL-HIMAYA ambayo ni fomula yenye ubora mkubwa kwa kuongeza CD4
    mwilini.

    Dawa hii inapatikana katika ofisi zetu za Arusha, Dar es Salaam, Mwanza na Kahama.

    Iwapo utakuwa na maswali kuhusu mwongozo zaidi kuhusu utengenezaji bora wa
    mchanganyiko wa kuongeza CD4 mwilini, unaweza kuwasiliana na Dr. Abdulkarim Mambo

    Saleh, Mobile phone: 0777 594334; 0658 594334.
    Pia unaweza kutembelea ofisi zetu ambazo anuani zake zimeandikwa nyuma ya jalada la
    kijitabu hiki.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom