Saimon Sayi "Complex"; Nyota iliyozimikia njiani. Alivuma zaidi katika nyimbo alizoshirikishwa kuliko za kwake!

Lavit

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2011
Posts
14,834
Reaction score
32,522
Sasa ni takribani miaka 12 toka atoweke duniani msanii na mtayarishaji maarufu wa muziki wa Bongo Fleva akijulikana kama Complex.

Jina la Complex lilianza kusikika hasa pale aliposhirikishwa na msanii mahiri kwa wakati huo akijulikana kama AY. Ay alimshirikisha Complex katika kibao chake cha Raha Tu Remix, hali iliyopelekea kujenga urafiki mkubwa baina ya hawa wawili.

Urafiki wa Ay na Complex ndiyo uliokuja kuwakutanisha Vivian na Complex, ikumbukwe kwamba hapo kabla tayari Ay na Vivi walikuwa wakifahamiana na ni Ay aliyefanya juhudi za kumkutanisha Vivi na Gadner na kupelekea kuajiriwa pale Clouds Media.

Complex aliweza kushirikishwa katika "hit songs" kama Nawakilisha (Prof J), Safari Njema (Jay Moe) , Njoo nikupe love (Bush Baby), Nimezama Remix (Ray C) , Hii Mic (TID) na Walidhani ya Zahrani.

Complex aliweza kufanya ngoma zake kama Hakuna hatari, Bab kubwa feat Jaydee, Wakati ndio huu feat Ay, Vita, Kufa na kupona pia Nyamaza aliyokuwa na Barish, Squeezer na Dataz. Mpaka leo hii Hakuna Hatari ndiyo ngoma iliyoacha kumbukumbu katika kazi zake mwenyewe.

Complex aliendelea na kazi ya Uproducer katika studio za Aigies na baadaye Backyards Studio. Wakati huo huo mpenzi wake Vivian aliweza kutoa ngoma kama Hip Hop muhimu akimshirkisha Ay, Siwaelewi akiwa na Dully pia kalamu na karatasi aliyoimba na Nuruely.

Tarehe 21 ya August mwaka 2005 ndiyo siku ambayo Complex na Vivi walipata ajari wakitokea Moro kwenye show ya Fiesta ambayo kwa wakati huo ilijulikana kama Moto zaidi, hiyo ndiyo ulikuwa mwisho wa safari ya hawa wawili katika muziki na mapenzi yao pia.


 
Ahsante kwa kunikumbusha wimbo nilioupenda sana kipindi kile. 'Hip hop muhimu', ngoja niutafute.
 
Mkuu utakuwa umechanganya mwaka....2015 ni juzi tu......2005 mbwewe.
 
Huyu jamaa nilitokea kumkubali [emoji817]

Nilikua naona msanii wa kwanza Tz kuvuka mipaka na kufanya colabs za nje na kuleta mafanikio mapema kabisa Tz, sema ndo hvyo tena ndoto ikazimika ghafla..

Mwenyenzi Mungu aipumzishe Roho ya Marehemu mahali panapostahili.
 
Nyamaza
Changa la macho
Raha tu
Halafu naskia yeye na Vivy walikuwa wamezaliwa tarehe zinazofanana ila Complex alikuwa kamtangulia mwaka.
Walikuwa pia safarini kutambulishana kwa wazazi walipopata ajali
 
vizuri huwa havidumu...
 
"Sisi tutakufa pamoja, wewe utakufa na nani? "

Hii ni kauli Vivian na Complex walipenda kumwambia jamaa mmoja(jina limenitoka) ambaye alikuwa rafiki yao wa karibu mno. Ndiyo hivyo maneno huumba, kweli wakaenda pamoja.
 

Hii ngoma ndio ipi hapo kwenye list yako ndugu...?
 

Attachments

Asante mkuu kwa kuweka kumbu kumbu hii muhimu sana katika historia ya muziki wa kizazi kipya...

Mungu awapumzishe pema huko walipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…