Saint Augustine University of Tanzania (SAUT) Special Thread

Revola

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2015
Posts
1,516
Reaction score
1,338
Wanajamii forums nimeanzisha uzi huu mahsusi kwa wanafunzi wote wa chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino Mwanza na campus Zoote za Tanzania. Tulio Maliza na tunaoendelea wote ni wanasaut. Karibuni tujadili mambo mbali mbali yahusuyo chuo tufahamiane na maisha ya chuo kwa ujumla. Karibuni sana.
SAUT WE BUILD THE CITY OF GOD.
Asante
 
Mkuu tuambie kuhusu saut campus ya Mwanza,,,mazingira,ubora wa elimu,makazi ya kuishi na gharama zake,chakula na upatikanaji wake,mahusiano ya kimapenzi(kwani nilisikia mliua MTU huko),fursa za kibiashara kwa mwanachuo na starehe
 
Mkuu tuambie kuhusu saut campus ya Mwanza,,,mazingira,ubora wa elimu,makazi ya kuishi na gharama zake,chakula na upatikanaji wake,mahusiano ya kimapenzi(kwani nilisikia mliua MTU huko),fursa za kibiashara kwa mwanachuo na starehe
Mazingira yako poa, gharama za msos na fuu ada inatofautiana kulingana na kozi lakin sio zaid ya 1.4m ila kama education 1.26m

Starehe na madem hayo ni mambo ya kawaida katika vyuo utafanya kadri upendavyo pia chuo hua kina leta wasanii mbalimbali ili kutoa burudan

Kuna Baadhi ya shoo kama Galanight ,Bonifire na zingine izo lazima ufurahie.

Wakufunzi wapo wa kutosha wengi masters ,kiasi dokta na maprofesa wapo.

Pia swala la msuli pale ni kawaida kushida chuo adi usku ni kawaida.
 
Ndo mana nilisema maelezo hayajatosha

Maelezo wote wanaosoma saut wanakijua ndio maana nikasema mwenye kukijua chuo atupia mambo yoote yahusuyo chuo Mimi nimemaliza saut 2011, ila fursa zipo biashara kama mchakalikaji unatoka kama mwanafunzi, mazingira ya chuo yapo vzr sn yanamfanya mwanafunzi avutiwe kusoma na kufanya fursa zingine.

Mfano chuoni nilipokuwa mwaka wa 2 baadhi ya wanafunzi walikuwa wanajishugulisha na maduka ya nguo, viatu, wengine walikuwa nadeal na laptop, wengine walipata fursa hata ya kufungua bar huku anasoma ilimradi tuu aingize kipato cha ziada huku anasoma na wengine waliweza kumiliki stationary zenye kila kitu kwa ajiri ya kusaidia wanafunzi wenzao kupata mahitaji na huduma za kimasomo.

Aidha kwa upande wa masomo zipo kozi nyingi zinaendeshwa Saut kwa msaada waweza tembelea www.saut.ac.tz hapo utapata kila kitu kuhusu kozi mbali mbali zitolewazo saut namengine meengi.

Ukija ktk upande wa accommodation chuo kimejipanga vizuri kuchukua wanafunzi wengi na mazingira ya uwekaji wa vyumba vya kulala vya wanafunzi vimejengwa vizuri sana na gharama za ulipiaji pia ni rafiki kwa mwanafunzi hazimuumizi mzazi katika kulipia, ila kwa watu wa HESLB wao hujilipia wenyewe bila wasi wasi, kwa upande wa mahusiano chuoni hapo siwezi kulisemea sn ila mahusiano chuo chochote yapo mkuu, ila wanafunzi wanajiheshimu kulingana na chuo chenyewe kilivyo.

Karibuni SAUT Malimbe ufurahie Elimu bora kwa maisha yako nayakizazi kijacho.
 
Du kila chuo thread ila sasa mbona hujatoa maelezo ya kushiba kuhusiana na chuo
Yes ni fursa mpya yakuweza kufahamiana zaidi, maisha yamekuwa tyt muda wa kutafutana umebana so kupitia hiki kitu twaweza juana kwa urahisi na update mbali mbali mkuu
 
Kama wewe ni Mwanafunzi njoo inbox nkupe fursa itakayo kufanya uishi Kama mfalme chuoni. Fursa itakayo kuwezesha na kukurahisishia Maisha yako hapo chuoni kiuchumi.

Uwe na smartphone tu.
Kwa nini usiziweke hapa kila mtu azijue mkuu??
 
Mkuu tuambie kuhusu saut campus ya Mwanza,,,mazingira,ubora wa elimu,makazi ya kuishi na gharama zake,chakula na upatikanaji wake,mahusiano ya kimapenzi(kwani nilisikia mliua MTU huko),fursa za kibiashara kwa mwanachuo na starehe
Sawa mkuu
 
Umenikumbusha born Fire mkuu hahaha nishida sn hapo aisee na FAWASCO
 
Unaweza uka-assess ubora wa chuo kwa kufuatilia watakayokuwa wanaongelea graduate na wanafunzi waliopo pale.
 
Hivi zile hostel za kule Darfull bado zipo??? Nimeishi pale darfull miaka yangu mitatu pindi nasoma Saut,nilikua chumba 210 next to my room alikua anaishi Bwana Moses Machali.... Kitima bado VC Saut?? Huyu jamaa ni mbabe hatari....

Kuna siku loan board walichelewa kulipa Schoo Fee, tukaenda kuongea na Kitima,tukamwambia Waziri wa Elimu kasema tufanya paper, serikali watalipa hela baadae, Jamaa alijibu kwa mkato hua naamulishwa na watu wawili tu, Papa na Kadinali Pengo, Mkitaka nimpigie hata Rais Kikwete muongee nae, Nimesema sitoi number hapa.....

Tukawa wapole kama sisimizi.... Bado kama lisaa limoja hivi kuanza paper....Jamaa ndo akaruhusu tupewe number....

Sasa wewe uko Malimbe, unachukua boda kwenda main campus kuchukua number,zen urudi malimbe kufanya paper....

Yaan huyo jamaa sitamusahau kabisa kwenye maisha yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…