Aramun
JF-Expert Member
- Nov 8, 2023
- 461
- 2,213
Kile ambacho ulimwengu wote umeona kama kashfa ya kanda ya ngono inaweza kuwa sehemu tu katika tamthilia ya maisha halisi kuhusu nani atakuwa rais ajaye wa Equatorial Guinea.
Katika muda wa wiki mbili zilizopita, video kadhaa - makadirio ni kati ya 150 hadi zaidi ya 400 - zimevuja za mtumishi mkuu wa serikali akifanya mapenzi ofisini kwake na kwingineko na wanawake tofauti.
Wanawake wengi waliorekodiwa walikuwa wake na jamaa za watu walio karibu na viongozi wa serikali kuu.
Inaonekana wengine walijua walikuwa wakirekodiwa wakifanya ngono na Baltasar Ebang Bw Engonga, ambaye pia anajulikana kama "Bello" kwa sababu ya sura yake nzuri.
Haya yote ni magumu kuthibitisha kwani Equatorial Guinea ni jamii yenye uminywaji wa habari ambapo hakuna vyombo vya habari huria.
Lakini nadharia moja ni kwamba uvujaji huo ulikuwa na nia ya kumchafua mhusika mkuu kwenye hizo kanda za video.
Soma Pia:
Bw Engonga ni mpwa wa Rais Teodoro Obiang Nguema na mmoja wa wale waliokuwa wanadhaniwa kuwa wanatarajia kuchukua nafasi yake.
Obiang ndiye rais aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi kuwahi kutawala tangu 1979.
Mzee huyo mwenye umri wa miaka 82 amesimamia ukuaji wa uchumi ambao umegeuka na kuwa mbaya kutokana na akiba ya mafuta ambayo sasa inapungua.
Kuna wasomi wadogo, matajiri sana, lakini wengi wa watu milioni 1.7 nchini wanaishi katika umaskini.
Utawala wa Obiang unakosolewa vikali kwa rekodi yake chafu ya haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na mauaji ya kiholela na mateso, kulingana na ripoti ya serikali ya Marekani.
Pia serikali yake imekuwa na sehemu yake ya kashfa - ikiwa ni pamoja na ufichuzi kuhusu maisha ya kifahari ya mmoja wa watoto wa kiume wa rais, ambaye sasa ni makamu wa rais, ambaye wakati mmoja alinunua glovu ya kioo ya $275,000 (£210,000) iliyovaliwa na Michael Jackson.
Glovu ya Bad Tour ya Michael Jackson iliwahi kumilikiwa na Makamu wa Rais Teodoro Obiang Mangue, ambaye ana nia ya kuwa Rais siku moja.
Licha ya uchaguzi wa mara kwa mara, hakuna upinzani wa kweli nchini Equatorial Guinea kwani wanaharakati wamefungwa na wengine kukimbia nchi na wale waliobakia wanafuatiliwa kwa karibu.
Siasa nchini humo kwa sasa zinahusu nani atafuatia kuingia ikulu na hapa ndipo kashfa inayomhusisha Bw Engonga ilipoibuka.
Bw Engonga Alikuwa mkuu wa Shirika la Kitaifa la Uchunguzi wa Fedha, na alifanya kazi katika kukabiliana na uhalifu kama vile utakatishaji fedha.
Lakini ikatokea yeye mwenyewe akawa chini ya uchunguzi.
Alikamatwa tarehe 25 Oktoba akituhumiwa kwa ubadhirifu wa kiasi kikubwa cha pesa kutoka kwenye hazina ya serikali na kuziweka kwenye akaunti za siri katika Visiwa vya Cayman. Hajasema lolote kuhusu tuhuma hiyo.
Kisha Bw Engonga alipelekwa katika gereza maarufu la Black Beach katika mji mkuu, Malabo, ambako inadaiwa kuwa wapinzani wa serikali huteswa.
Simu na kompyuta zake zilinaswa na siku chache baadaye video hizo zikaanza kuonekana mtandaoni.
Bw Engonga alitambuliwa haraka pamoja na baadhi ya wanawake katika video hizo, wakiwemo jamaa za rais na wake wa mawaziri na maafisa wakuu wa kijeshi.
Serikali haikuweza kupuuza kilichokuwa kikiendelea na tarehe 30 Oktoba Makamu wa Rais Teodoro Obiang Mangue (aliyewahi kuwa mmiliki wa glovu ya Michael Jackson) alizipa kampuni za mawasiliano masaa 24 kuja na njia za kukomesha uenezaji wa klipu hizo.
"Hatuwezi kuendelea kutazama familia zikisambaratika bila kuchukua hatua yoyote," aliandika kwenye X.
"Wakati huo huo, chanzo cha machapisho haya inachunguzwa ili kuwapata waliovujisha na kuwawajibisha."
Kwa kuwa vifaa vya kompyuta vilikuwa mikononi mwa vikosi vya usalama, tuhuma inamwangukia mtu ambaye, labda, alitaka kuharibu sifa ya Bw Engonga kabla ya kesi.
Polisi wametoa wito kwa wanawake kujitokeza kumfungulia kesi Bw Engonga ya kusambaza picha za siri bila maelewano. Mmoja tayari ametangaza kwamba anamshitaki.
Jambo ambalo halijabainika ni kwa nini Bw Engonga alirekodi klipu hizo.
Lakini wanaharakati wameweka mbele kile ambacho kinaweza kuwa nia nyingine nyuma ya uvujaji wa klipu hizo.
Pamoja na kuwa na uhusiano na rais, Bw Engonga ni mtoto wa Baltasar Engonga Edjo'o, mkuu wa muungano wa kiuchumi na kifedha wa eneo hilo, Cemac, na mwenye ushawishi mkubwa nchini humo.
"Tunachoona ni mwisho wa enzi, mwisho wa rais wa sasa, na kuna mfululizo [swali] na haya ni mapigano ya ndani tunayoona," mwanaharakati wa Equatoguine Nsang Christia Esimi Cruz, ambaye sasa anaishi London. .
Akizungumza na podikasti ya BBC Focus on Africa, alidai kuwa Makamu wa Rais Obiang alikuwa akijaribu kumuondoa kisiasa "mtu yeyote ambaye angeweza kupinga urithi wake".
Makamu wa rais, pamoja na mama yake, wanashukiwa kuweka kando mtu yeyote anayetishia njia yake ya urais, akiwemo Gabriel Obiang Lima (mtoto mwingine wa Rais Obiang kutoka mke tofauti), ambaye alikuwa waziri wa mafuta kwa miaka 10 na kisha kuhamishwa kutoka serikali kuu.
Teodoro Obiang Mangue (kushoto) alikua Makamu wa Rais tangu mwaka 2016.
Lakini Bw Cruz pia anadai kuwa mamlaka inataka kutumia kashfa hiyo kama kisingizio cha kukandamiza mitandao ya kijamii.
Mnamo Julai, mamlaka ilisimamisha mtandao kwa muda baada ya maandamano kuzuka katika kisiwa cha Annobón.
Kwake, ukweli kwamba afisa wa ngazi ya juu alikuwa akifanya ngono nje ya ndoa haikushangaza kwani ilikuwa ni sehemu ya maisha machafu ya wasomi na viongozi wa nchi hiyo.
Makamu huyo wa rais ambaye yeye mwenyewe alituhumiwa kwa ufisadi nchini Ufaransa na kunyang'anywa mali za kifahari katika nchi mbalimbali, anataka aonekane ndiye mtu anayepambana na ufisadi na maovu nyumbani.
Mwaka jana, kwa mfano, aliamuru kukamatwa kwa kaka yake wa kambo kwa madai ya kuuza ndege inayomilikiwa na shirika la ndege la serikali.
Lakini katika kesi hii, licha ya juhudi za makamu wa rais kukomesha kuenea kwa video, zimeendelea kusambaa na kutazamwa.
Wiki hii, alijaribu kuonekana dhabiti zaidi akitoa wito wa kufungwa kwa kamera za CCTV katika ofisi za serikali "ili kukabiliana na vitendo vichafu na visivyo halali", shirika rasmi la habari liliripoti.
Akisema kwamba kashfa hiyo "imedhalilisha sura ya nchi" aliamuru kwamba maafisa wowote watakaopatikana wakijihusisha na vitendo vya ngono kazini watasimamishwa kazi kwani huo ulikuwa "ukiukaji wa wazi wa kanuni za maadili".
®BBC

- Guinea: Kigogo anaswa na video 400 za ngono na wake wa viongozi mashuhuri, mwanasheria Mkuu aingilia kati
- Mwanamke mmoja miongoni mwa waathirika wa kashfa ya ngono ajiua kuepuka aibu ya Baltasar Engonga aliyenaswa na Video 400 za ngono na wake wa viongozi