Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Kadinali Pengo na Mzee Kutima wanawakilisha wanazuoni wa kidini wanaokubaliana na tahadhari ya Dr. Freeman Mbowe kwenye sakata la kukodishwa Bandari. Mzee wetu pengo kwa unyenyekevu mkubwa anawauliza watawala " Mmepewa madaraka mtupatie fedha nyingi au Mmepewa madaraka mtujengee uwezo wa kujitegemea" . Kwa tafsiri nyepesi Mzee Pengo anawauliza watawala kwanini wanaoana fahari kutuuza utumwani kwa kuona hatua na uwezo wa kujitegemea?
Kijamii Mzee Pengo anawauliza watawala; ni lini wamewahi kutuliza kama tunaweza kujitawala tukasema hatuwezi tunataka kutawaliwa? Lakini pia anatuuliza kama watawala wamejaza ndugu zao kwenye kila eneo nyeti la nchi hii na hao ndugu zao wameshindwa kujitegemea je ndo kusema Watanzania wote tumeshindwa kujitegemea tunatakiwa kutawaliwa? Kwanini watawala wasingeamua kwa dhati kabisa kuondoa ndugu zao kwenye nafasi za juu za tawala wakaruhusu damu mpya tuonyeshe kwamba watanzania hatujafeli badi ndugu za watawala ndio waliofeli?
Haya maswali ndiyo aliyouliza Mhe. Mbowe Daktari wa siasa nchini.
Kwa upande wa pili wananchi wote wanauliza kama alivyouliza Mbowe kwamba ni kweli tupo tayari kama Taifa kuruhusu watu wachache wauze bandari zetu? Kama kila mwananchi anapinga suala hili nani amewatuma watawala? Je. Wao wana uchungu zaidi kuliko wananchi? Toka lini wakaanza kuwa na uchungu kuliko wananchi?
Mwisho kwenye vyombo vya usalama; naamini viongozi wa dini waliopinga suala hili wametumwa na viongozi wa usalama wa Taifa letu, naamini wanazungumza kwa niaba ya wananchi; naamini wameona kabisa ndugu na watawala waliokabidhiwa jukumu la kumshauri mtukufu Rais awafanyi kazi yao; wameona kabisa ofisi za wizara hasa miundombinu na ofisi ya AG hazina wataalam bali zina watoto wa wakubwa ambao kwa kuwa wao wanakula na wamekula wakila na kusaza toka utotoni basi kwao kuuza nchi shida kwa sababu wanao mtaji wa kisiasa na watarithishana madaraka milele.....
Hongera Mhe. Mbowe umetimiza wajibu, Hongera Kutima, hongera mzee wetu Pengo..........historia itawakumbuka.
Naamini hakuna mtu ambaye anateseka kwenye nafsi wakati huu kama Mzee Mbarawa; for about two weeks now anazunguka kuongea na watu japo anachokiongea sehemu A hakiendani na sehemu B. Naamini katika maisha yake hakuwahi kuwaza kwamba angeweza kufanya kosa kama hili.......wengine jifunzeni kujipa muda wa kutosha kujadili na kusoma mnachotaka kusaini