MUSHEKY
JF-Expert Member
- May 9, 2014
- 2,812
- 2,760
Bila salamu nijielekeze moja kwa moja kwenye mada
Kama binadamu (sio robot) leo nimeona nitimize wajibu wangu kuongea machache yanayohusiana na sakata la hizi bandari zetu
Kwanza kabisa niwakumbushe watawala wote (hasa wale wa ngazi zinazonyenyekewa) akiwemo Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwamba rasilimali zote zilizomo kwenye nchi hii ni mali za asili za Watanzania wote na hakuna kundi miongoni mwetu lenye haki zaidi ya jingine juu ya zawadi hizi alizotupa bure Muumba wetu kwa mapenzi yake matukufu.
Taratibu za nchi zote duniani kama tulivyofanya sisi ni kumtafuta kiranja mkuu na viranja wengine wasaidizi na KUWAAMINI kuwakabidhi amana zetu hizi wazitunze na kuziendeleza kwa woga na unyenyekevu mkubwa kwa ajili ya vizazi vyetu vya muda tulionao na vile vitakavyokuja wakati sisi tukishatoweka hapa duniani huku pia wakitambua kua watanzania WOTE tungetamani kushika nyadhifa za juu hata kwa wiki moja moja kupokezana ili kila mmoja wetu aandike historia ya kuongoza na kudhibiti keki zetu hizi adimu ambazo kila mmoja wetu ana shea sawa na mwingine lakini kwa kutumia akili ya kawaida jambo hilo ni gumu ndipo tukaiacha busara itawale na tuwaamini wenzetu wachache mtuongoze njia.
Baada ya kusema hayo lipo la kuiga kwa wenzetu huko duniani waliotutangulia hasa linapokuja suala la kutanguliza maslahi ya taifa mbele.
Nyie viongozi wetu mnapoona mmependekeza jambo mnalodhani lina maslahi pana kwa watu wote(ambao kimsingi ndio wenye nchi) kisha mkapata kupingwa kwa kiasi kikubwa na UMMA(wenye mali zao) basi mnapaswa kurudi nyuma na kuwasikiliza wanachotaka (kuchutama) kwa kua.
1. Wao ndio wenye mali yao
2. Nyie ni viranja tu wa kusimamia
3. Wenye mali zao (wananchi) wana
Akili na uelewa mpana juu ya mali zao
Boris johnson wa Uingereza baada ya kukosa uungwaji mkono na waingereza kwenye kile alichokiwaza kama kiongozi wa taifa hilo alionyesha uwajibikaji kwa kua alijua wenye nchi yao (waingereza) wana maamuzi mapana zaidi ya nchi yao kuliko yeye (BORIS) na kikundi cha viranja wenzie wachache.
Sisemi rais ajiuzulu kama Boris laa! Ila zipo namna mbalimbali za kuwanyenyekea unaowatawala kuwaonyesha kwamba umewasikia na unathamini kile wanacho na wasichokitaka kifanyike kwenye rasili
mali zao
Sidhani sana kama ni busara kutumia "mbinu" ya kuziba masikio na vijembe vya rejareja juu ya wale wenye maoni kinzani.
Tanzania ni yetu sote tuijenge kwa pamoja.
Muungwana akivuliwa nguo anachutama.